Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salah hatihati kukosa mechi zilizobakia Liverpool

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo raia wa Misri amefunga idadi ya mabao 257 katika mechi 440 za mashindano yote akiwa na Liverpool.

Liverpool, England. Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah huenda akakosekana katika mechi zilizobaki za kumaliza msimu wa Ligi Kuu England akiwa ndani ya uzi wa Majogoo wa Anfield baada ya kupata jeraha la msuli wa paja litakalomweka nje hadi mwisho wa msimu.

Taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa timu ya taifa ya Misri, Ibrahim Hassan, zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo amepata mchubuko mkubwa kwenye misuli hiyo na atahitaji takribani wiki nne kupona.

Jeraha hilo lina maana kuwa mshambuliaji huyo atakosa mechi zote zilizobaki mwezi Mei, hatua inayozima matumaini ya kuaga mashabiki wa Anfield uwanjani, hasa ikizingatiwa kuwa anatarajia kuondoka klabuni hapo majira ya kiangazi baada ya kuitumikia kwa miaka tisa.

Meneja wa Liverpool, Arne Slot, amekiri kutokuwa na uhakika kamili wa hali ya nyota huyo, lakini ameonyesha uwezekano mdogo wa kurejea kabla ya msimu kumalizika.

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah akionekana kushika paja la kushoto akiashiria maumivu wakati wa mechi ya Ligi Kuu England iliyopigwa Jumamosi Aprili 25, 2026 kwenye Uwanja wa Anfield dhidi ya Crystal Palace. Kulia ni Meneja wa timu hiyo Arne Slot Picha na Mtandao

“Hatujui kwa uhakika. Muda uliobaki wa msimu ni mfupi sana, hivyo tunasubiri kuona hali itakavyokuwa,” amesema Slot.

Licha ya pigo hilo, taarifa zinaeleza kuwa Salah anatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Marekani, Canada na Mexico jambo litakalokuwa faraja kwa timu ya taifa ya Misri.

Kwa sasa, Liverpool wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na wana nafasi kubwa ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Iwapo Salah hatacheza tena msimu huu, itakuwa mwisho wa enzi muhimu kwa mmoja wa wachezaji walioandika historia kubwa ndani ya Liverpool huku mashabiki wakibaki na kumbukumbu ya mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo.