Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu mastaa Yanga kuitwa kambini

Muktasari:

  • Hamdi amewaita nyota wake kwa ajili ya kujiweka tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida Black Stars. Kocha huyo amesema hana kawaida ya kuhofia mchezaji wa timu pinzani

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga, Hamdi Miloud amewaita haraka wachezaji wake kambini tayari kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kuifuata Singida Black Stars.

Mchezo huo dhidi ya Sindida ni wa kirafiki na maalumu kwa ajili ya kuzindua uwanja utakaokuwa unamilikiwa na Singida Black Stars.

Hamdi amewaita nyota wake wote ambao hawajaitwa kwenye vikosi vyao vya timu ya taifa kwa ajili ya kujiweka tayari na safari ya kwenda Singida kesho Machi 22, 2025 kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumatatu ijayo.

Akizungumza na Mwananchi kocha huyo, amesema ni mchezo muhimu kwao kutokana na timu hiyo kushindwa kupata muda wa kucheza tangu ulipoahirishwa mchezo wao dhidi ya watani zao Simba huku akisisitiza kuwa ni wakati sahihi wa wachezaji wake kuonyesha uwezo hasa wale ambao wamekuwa wakikosa nafasi ya kucheza.

"Natarajia mchezo mzuri na bora kutoka kwa Singida Black Stars kutokana na kuwa na nyota wengi bora na wazoefu, naifahamu vizuri timu hiyo pamoja na kwamba sipo hapa nchini muda mrefu.

"Ni kipimo kizuri kwetu na ni muda sahihi kupimana nao nguvu na kubaini ubora wao na mapungufu yao yakiwa ni maandalizi sahihi ya michezo yetu ijayo ya ligi," amesema kocha huyo.

Hamdi amesema hana kawaida ya kuhofia mchezaji wa timu pinzani, anatishika na mbinu za makocha uchezaji ni namna ambayo mchezaji mmoja mmoja anaonyesha ubora wake.

"Sina kawaida ya kumhofia mchezaji yeyote, natambua ubora wao lakini mbinu sahihi ndio zinaamua matokeo pale wachezaji 22 wanapokutana, nakiamini kikosi changu na nawaheshimu wapinzani."

Yanga kwenye kikosi chao wanatarajia kuwakosa Djigui Diarra, Dickson Job,  Ibrahim Hamad 'Bacca', Khalid Aucho, Duke Abuya, Clatous Chama, Kennedy Musonda, Mudathir Yahya, Prince Dube na Clement Mzize ambao wameitwa na timu zao za taifa.

Hivyo nyota wengine wote wa kikosi hicho waliosalia watakuwa sehemu ya wale watakaoondoka jijini Jumamosi ya wiki hii tayari kwa mchezo huo.

Hii itakuwa timu ya nne kwenye Ligi Kuu Bara kumiliki uwanja baada ya Azam, JKT Tanzania pamoja na KMC Complex.