Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rio Ferdinand aanika sababu za kutua Tanzania wiki ijayo

Beki wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya England, Rio Ferdinand. Picha na Mtandao

Beki wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya England, Rio Ferdinand amesema kuwa ameshawishika kuja nchini wiki ijayo kwa vile Tanzania ni nchi nzuri na inayopenda soka.

Ferdinand amesema hayo kupitia video aliyorekodi kuelezea ujio wake nchini siku ya Jumanne, Mei 19, 2026.

Nyota huyo aliyetwaa mataji 14 katika miaka 12 aliyoichezea Manchester United, amesema kuwa baada ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameamua kufanya ziara hiyo nchini ambayo pia anaamini itafungua fursa mbalimbali.

“Ninatazamia kutembelea Tanzania wiki ijayo baada ya kuwa na mazungumzo mazuri na Waziri Paul Makonda pamoja na wengine kuhusu makubwa yaliyopo ndani ya nchi.

“Kwangu mimi, safari hii inahusu watu, utamaduni, soka na fursa. Tanzania ina shauku kubwa sana kwa michezo na ina kizazi cha vijana chenye hamasa kubwa, na ninatazamia kwa dhati kujifunza zaidi, kukutana na watu moja kwa moja na kutazama jinsi tunavyoweza kujenga fursa zenye maana pamoja katika siku zijazo.

Beki wa zamani wa Manchester United na England, Rio Ferdinand. Picha na Mtandao

“Ni heshima sana kupata fursa ya kukutana na Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa ziara yangu, na ninafurahia kupata uzoefu zaidi kuhusu nchi hii nzuri.

Beki huyo wa kati ni miongoni mwa wachezaji waliopata mafanikio makubwa kwa kutwaa idadi kubwa ya mataji katika ngazi ya klabu. Idadi kubwa ya mataji ambayo Ferdinand amenyanyua ni ndani

ya Manchester United ambapo katika kipindi cha miaka 12 aliyoichezea, timu hiyo ilinyakua mataji 14 tofauti.

Beki wa zamani wa Manchester United, West Ham na timu ya Taifa ya England, Rio Ferdinand. Picha na Mtandao

Mataji sita ni ya Ligi Kuu England, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, moja la Klabu Bingwa ya Dunia, manne ya Ngao ya Jamii na mawili ya Kombe la Ligi.

Akiwa na West Ham, Rio Ferdinand alitwaa taji la UEFA Intertoto mwaka 1999.

Mafanikio binafsi ya Ferdinand katika soka ni pamoja na kuingia katika kikosi bora cha Dunia cha FIFA mara moja na kuwemo katika Kikosi bora cha Ligi Kuu England mara sita.