Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Remix ya Seduce Me yanukia

Muktasari:

  • Wimbo huo wa Alikiba umepata mafanikio makubwa katika mitandao ya kijamii

Dar es Salaam. Wakati nyimbo ya Seduce Me ya Alikiba ikiendelea kukimbiza katika kumbi na mitandao ya kijamii kuna taarifa zinadai  kuwepo kwa mpango wa Remix.

Nyimbo hiyo hadi sasa imepata watazamaji 6.8 milioni kwenye mtandao wa Youtube.

Akizungumzia suala hilo mtayarishaji wa nyimbo hiyo, Man Walter alisema uwezekano upo, lakini anasubiri mwenye wimbo aamue cha kufanya.

“Kama Ali Kiba ataamua mwenyewe itakuwa sawa na naona si lazima ifanyike katika mfumo wa rege kama sasa, inaweza kufanyika kinamna tofauti na bado inaweza kufanya vizuri sababu ni wimbo wa watu,” alisema.

Pia, produza huyo aliongeza kuwa mafanikio ya wimbo huo kwake imekuwa ni kitu cha kushangaza sababu ni kitu ambacho walikiandaa kwa ukawaida sana.

“Ngoma mpaka sasa mimi nashangaa mafanikio yake, lakini naamini hii kweli ni ngoma ya watu, watu ndio wameifanya mpaka hapo ilipo,” aliongeza.