Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yatibua dili la Zubimendi Arsenal

ZUBI Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Arsenal ina imani wameshaweka msingi wa kumsajili Zubimendi kutoka Real Sociedad dirisha lijalo.

LONDON, ENGLAND: Licha ya Arsenal kuripotiwa imeshafanya makubaliano ya kumsajili Martin Zubimendi dirisha lijalo, ripoti zinadai mkurugenzi mpya wa michezo, Andrea Bertilazima aendelee kupigana na Real Madrid ambayo imeibuka hivi karibuni kutaka kumsajili.

Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, Arsenal ina imani wameshaweka msingi wa kumsajili Zubimendi kutoka Real Sociedad dirisha lijalo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania ana kipengele katika mkataba wake kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 51 milioni na Arsenal ambayo imekuwa ikimfuatilia kwa miezi 18, ipo tayari kukilipa.

Mazungumzo baina ya Sociedad na Arsenal yalianza tangu mwaka jana na sasa anayetakiwa kumaliza kazi ni mkurugenzi mpya wa michezo Berti kumaliza makubaliano hayo.

Madrid bado haina uhakika juu ya mustakabali wa kocha wao na wanahusishwa kutaka kumwajiri Xabi Alonso ambaye kama atapewa mikona itakuwa habari mbaya kwa Arsenal juu ya dili lao la Zubimendi kwani kocha huyo ana uhusiano naye wa karibu.

Zubimendi mwenye umri wa miaka 26, alijenga uhusiano na Xabi pale kocha huyo alipokuwa Sociedad ya vijana kabla hajatimkia Bayer Leverkusen.

Katika maisha yake ya soka, Zubimendi amecheza mechi 15 za timu ya taifa na amecheza mechi 227 katika kikosi cha  Sociedad ambacho ana mkataba wa kuhudumu hadi mwaka 2027.