Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi waeleza sababu za kuendelea kumshikilia Mwakinyo

Muktasari:

  • Bondia Mwakinyo anatuhumiwa kumshambulia kijana anaejulikana kwa jina la Mussa Ally ,akiwa nyumbani kwake na kumjeruhi maeneo mbalimbali ya mwili wake, na sasa anaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa ya Bombo.

Tanga. Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limeeleza sababu za kuendelea kumshikilia bondia maarufu nchini, Hassan Mwakinyo (29), anayetuhumiwa kumshambulia mkazi wa jijini humo, Mussa Ally akimtuhumu kuwa ni mwizi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu Machi 10, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema Mwakinyo anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi Mussa, ambaye anajishughulisha na uvuvi kwa madai kuwa alipopita kwenye makazi yake.

Kamanda Mchunguzi amesema kuwa uchunguzi wa tuhuma hizo unaendelea na kwamba, watatoa taarifa rasmi na hatua zinazofuata pindi utakapokamilika.

"Tunamshikilia mkazi wa Sahare jijini Tanga, Hassan Mwakinyo kwa kumshambulia na kumjeruhi Mussa Ally. Uchunguzi wa tukio hili unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atapelekwa mahakamani," amesema Mchunguzi na kuongeza: “Tunatoa wito wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuacha kujihusisha na vitendo viovu hasa matukio ya kujichukulia sheria mikononi kwani, kwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.’

Kwa mujibu wa Kamanda Muchunguzi amesema Mwakinyo baada ya kuhojiwa, amedai kuwa alimchukulia mtu huyo kama mwizi.

Tukio hilo lilitokea Machi 4, 2025 katika eneo la Sahare ambako ndiko makazi ya Mwakinyo.