Wachezaji 36 wapewa kadi nyekundu
ASUNCION, Paraguay
WACHEZAJI 36 pamoja na wale wa akiba wa timu zote mbili, walitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi kwenye mchezo wa Ligi ya vijana nchini Paraguay.
Katika dakika tano za mwisho za mchezo huo wa Jumapili, mwamuzi Nestor Guillen alitoa kadi nyekundu wachezaji wawili waliokuwa wakipigana, lakini wawili hao waliendelea kupigana ndani ya uwanja pamoja uamuzi wake.
Kutokana na tukio hilo wachezaji wengine wakaamua kuingia kati na kuzusha kasheshe uwanjani hapo.
"Wachezaji wote waliingia uwanjani pamoja na wale wa akiba na kuanza kupigana na wengine wakijaribu kugombelezea wasiendelee kupigana," alisema Hernan Martinez ambaye ni rais wa timu ya Teniente Farina.
Badala ya kujaribu kumaliza tatizo hilo, waamuzi wa mchezo huo waliamua kukimbia kiwanjani kwa uoga.
Kwa sababu hiyo, Martinez anaamini mwamuzi hakuwa na kufanya zaidi ya kutoa kadi nyekundu kwa wachezaji wote 36, kwa kuwa hakubaki uwanjani ili kuwatambua wachezaji waliofanya vurugu.
"Waamuzi hawakubaki uwanjani kuona nini kinatokea. Baada ya vurugu kuanza walikimbilia kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo," alisema.
Rais wa wageni Libertad, Sixto Nunez alisema mwamuzi alishindwa kutimiza jukumu lake.
"Mwamuzi alitakiwa kuwaelekeza hawa watoto. Alitakiwa kuhakikisha wale wachezaji wawili walioanza kupigana wanatoka nje ya uwanja kabisa," alisema Nunez.
"Pamoja na mwamuzi kuondoka uwanjani na kuwaacha wachezaji pekeo yao nadhani imechangia kuendelea kwa vurugu hizo," aliongeza.
Wachezaji wote wamefungiwa na sasa wanasubiri adhabu zaidi kutoka kwa Kamati ya Nidhamu ya ligi.