Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marekani, China zafunga kibabe Olimpiki 2024

Muktasari:

Nchi kadhaa zimeonyesha uwezo wa juu kwenye mashindano hayo yaliyofanyika nchini Ufaransa kwenye mji wa Paris.

Paris, Ufaransa

Mashindano ya Olimpiki yamemalizika usiku wa kuamkia leo huku nchi za Afrika zikishindwa kufanya vizuri kwa mwaka huu.

Nchi kadhaa zimeonyesha uwezo wa juu kwenye mashindano hayo yaliyofanyika nchini Ufaransa kwenye mji wa Paris.

Marekani imemaliza ikiwa kinara wa nchi iliyochukua medali nyingi zaidi kwenye mashindano ya mwaka ikiwa imechukua jumla ya medali 126.

Katika medali hizo za dhahabu ni 40 ikifuatiwa na China ambayo imechukua jumla ya medali 90, lakini ikiwa imefanya vizuri kwenye zile za dhahabu baada ya kukusanya 40 sawa na Marekani.

Jambo la ajabu ni gepu kubwa ambalo limeonekana kutoka kwenye nchi ya pili na ile iliyoshika nafasi ya tatu ambayo ni Japan iliyokusanya jumla ya medali 45 nusu ya nchi iliyoshika nafasi ya pili, lakini Japan imefanikiwa kukusanya zile za dhahabu 20 zikiwa pia ni nusu ya ilizochukua Marekani na China ambazo zimeshika nafasi ya kwanza na ya pili.

Nchi ya Afrika iliyofanya vizuri zaidi kwenye medali hizo ni Kenya ambayo ipo nafasi ya 17 ikiwa imekusanya jumla ya medali 11 zikiwemo za dhahabu nne,  ikifuatiwa na  Algeria iliyopo nafasi ya 39 baada ya kuchukua jumla ya medali tatu zikiwemo mbili za dhahabu.

Afrika Kusini ndiyo inafuata ikiwa nafasi ya 44 baada ya kukusanya medali sita ikiwemo moja ya dhahabu, ikifuatiwa na Ethiopia yenye medali nne moja ikiwa ya dhahabu.

Zaidi ya nchi 120, zimetoka kwenye mashindano haya bila kutwaa medali yoyote.

Wakati wa sherehe za kufunga mashindano hayo ya 33, walihudhuria watu maarufu akiwemo mwigizaji Tom Cruise na wasanii wa muziki Chili Peppers, Billie Eilish, Snoop Dogg  na Dr Dre ambao walifanya shoo matata sana.

Akifunga mashindano hayo rais wa kamati ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach, alisema anaamini haya ni mashindano bora zaidi kuwahi kutokea.

Bach, ambaye ataachia ngazi mwaka 2025, amesema mashindano hayo ya Paris yalikuwa bora sana na kuonyesha picha halisi ya jinsi ambavyo Olimpiki inatakiwa kuandaliwa.

Pia bosi huyo alipongeza jinsi ambayo kumekuwa na mgawanyo sawa wa wanawake na wanaume kwenye mashindano ya mwaka huu tofauti na jinsi ilivyokuwa huko nyuma.

“Haya yalikuwa mashindano bora sana na niwapongeze watu wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine.

“Kwa kipindi chote tulichokuwa hapa Paris tuliishia kwa amani upendo na furaha, tuliheshimiana, hii ndiyo maana halisi ya mashindano ya Olimpiki.

“Hali hii inawavutia mabilioni ya watu duniani kote, asante kwa kuifanya hii ndoto kuwa kweli, asanteni kwa kujali maisha ya watu wote duniani,” alisema bosi huyo.

Hata hivyo, alisema anafurahi kwa kasi kubwa iliyofanyika akiamini kuwa mashindano yatakayofanyika nchini Marekani kwenye mji  wa Los Angeles, mwaka 2028 yatakuwa bora zaidi.