Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yarudi Aston Villa kumchomoa Martinez

MARTINEZ Pict

Muktasari:

  • Martinez alikuwa na ‘hamu kubwa’ ya kutua Old Trafford na kuwa kipa namba moja wa Man United

MANCHESTER, ENGLAND: Makosa yaliyoonyeshwa na makipa wawili wa Manchester United, Andre Onana na Altay Bayindir hivi karibuni, yamesababisha mabosi wa mashetani hao wekundu kurudi kubisha hodo Aston Villa kabla dirisha la usajili halijafungwa ili kuinasa saini ya kipa wao, Emiliano Martinez.

Bayindir ambaye amekuwa akiaminiwa kusimama langoni katika mechi za Ligi Kuu England huku Onana akidaka mchezo wa Kombe la Carabao walikoondoshwa na timu ndogo ya Grimsby Town FC kwa mikwaju 12-- baada ya sare ya mabao 2-2, wameonekana hawana maajabu kusimama lango la miamba hiyo ya Old Trafford.

Na sasa Man United ambayo imekuwa ikiruhusu mabao katika mechi ilizocheza hivi karibuni ikiwamo ya juzi Jumapili ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Burnley, imeonyesha wazi inataka kipa mwingine kabla dirisha halijafungwa na imetuma ofa dakika za mwisho ili kumsajili kipa Martinez.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za uhamisho Fabrizio Romano, viongozi wa Man United wamefanya mawasiliano upya na Martinez ambaye awali mwanzoni mwa dirisha hili waliripotiwa kutaka kumsajili kabla ya kuachana na mpango huo.

Kipa huyo wa kimataifa wa Argentina,32, alionekana kuwaaga mashabiki wa Villa mwishoni mwa msimu uliopita na aliripotiwa angetua Man United lakini uhamisho haukutimia.

Martinez alikosa mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi ya Newcastle kutokana na adhabu ya kufungiwa, lakini alirudi langoni katika kipigo cha 1-0 dhidi ya Brentford wiki iliyopita.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia bado ana mkataba wa miaka minne na Villa, ambao aliusaini miezi 12 iliyopita.

Hata hivyo, Juni mwaka huu tovuti ya ESPN ilidai Martinez alikuwa na ‘hamu kubwa’ ya kutua Old Trafford na kuwa kipa namba moja wa Man United na mashetani hao wekundu walituma hadi ofa ya kutaka kumsajili kwa mkopo lakini ikakataliwa na mabosi wa Villa.

Mbali na Martinez mwenye urefu wa futi 06 na inchi 05, viongozi wa Man United pia wanamuwinda kipa wa Antwerp, Senne Lammens na wamekuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na klabu hiyo ya Ubelgiji kuhusu mchezaji huyo.

Lammens alianza mechi nne za kwanza za msimu akiwa langoni mwa Antwerp, lakini wiki iliyopita aliondolewa kwenye kikosi cha mechi kutokana na tetesi za uhamisho.

Nguli wa Old Trafford na aliyewahi kuichezea Villa, Dwight Yorke, 53, anaamini Martinez ndiye mtu sahihi kwa Man United.

Akihojiwa na Jackpot City Casino, Yorke alisema: “Emi Martinez ana umbo kubwa, hilo halina kificho. Amechukua Kombe la Dunia, ni miongoni mwa makipa bora sana linapokuja suala la kuokoa mikwaju ya penalti, yaani ana kila kitu. Niliamini kabisa tungepata saini yake kwa sababu ilionekana kama alikuwa karibu mno kuhamia Man United. Labda alijaribu kulazimisha uhamisho huo, lakini kwa sababu fulani haukutimia.”

“Hata hivyo, Villa pia ni klabu ninayoifahamu vyema, hivyo kama ataendelea kubaki pale, bado ni uamuzi mzuri kwake.”