Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeraha yamtupa nje Masaka WAFCON

Muktasari:

  • Utakumbuka Novemba 09 mwaka jana Masaka alipata jeraha la bega kwenye mchezo wa Ligi Kuu England (W) dhidi ya Arsenal na baada ya hapo hakupata nafasi ya kucheza tena msimu mzima.

Mshambuliaji wa Brighton ya England na timu ya taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Aisha Masaka hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachocheza mashindano ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON), wikiendi hii nchini Morocco.

Katika mashindano hayo ambayo yataanza Julai 5-26, Twiga Stars imepangwa Kundi C ikiwa pamoja na vigogo, Mali, Ghana na Afrika Kusini.

Masaka ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo zaidi kwenye kikosi cha Twiga Stars na alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwika kwenye mashindano hayo makubwa kwa wanawake barani Afrika.

Akizungumzia kuhusu kukosekana kwake Masaka amesema kuwa alitamani sana kuwemo kwenye michuano hiyo lakini jeraha la goti limekatisha ndoto hiyo.

"Ni vigumu kuelezea kwa maneno machungu ninayoyahisi sasa, Lakini itoshe kusema kwa ufupi michuano ya WAFCON ilikuwa ndoto niliyoitamani kwa muda mrefu ndoto ya kuvaa jezi ya taifa langu na kupambana bega kwa bega na wenzangu kwa ajili ya bendera yetu," aliandika Aisha na kuongeza;

"Kwa bahati mbaya, majeraha ya goti niliyoyapata wakati wa maandalizi ya mwisho kuelekea fainali hizi, pamoja na mashindano ya CECAFA, yamezima ndoto hii. Ni maumivu makubwa sana kwangu siyo tu kimwili, bali zaidi kiakili na kihisia kwa sababu najua ni jambo nililoliombea na kulifanyia kazi kwa muda mrefu.

"Lakini naamini kila jambo hutokea kwa sababu, na mapenzi ya Mungu daima ni makubwa kuliko mipango yetu binadamu, Nitaendelea kupigania kupona na kurejea uwanjani nikiwa na nguvu mpya, moyo mpya, na ari kubwa kuliko awali."

Nyota huyo wa zamani wa Yanga Princess na BK Hacken ya Sweden aliongeza; "Ninawashukuru kwa dhati mashabiki, familia, marafiki na wenzangu kwa sala, upendo na maneno yenu ya kunitia moyo, Sapoti yenu inanipa sababu ya kuendelea kusimama imara na kutokata tamaa.

"Naamini wachezaji wenzangu wataendelea kupambana kwa moyo wote na kulitumikia taifa letu kwa fahari kubwa, kama walivyofanya kwenye michuano ya CECAFA. Let’s go Twiga Stars!Watanzania wote tuko nyuma yenu, tunawatakia kila la heri na mafanikio kwenye michuano hii." aliandika hivyo

Utakumbuka Novemba 09 mwaka jana Masaka alipata jeraha la bega kwenye mchezo wa Ligi Kuu England (W) dhidi ya Arsenal na baada ya hapo hakupata nafasi ya kucheza tena msimu mzima.