Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yaanza kumsaka mrithi wa Salah, yakwama kwa Olise

Muktasari:

  • Baada ya Salah kutangaza kuondoka kwenye viunga vya Anfield mwishoni mwa msimu huu, Liverpool imeanza kumtafuta mbadala wake haraka huku ikikumbana na kikwazo Ujerumani.

London, England. Klabu ya Liverpool imekumbana na kizingiti katika harakati zake za kutafuta mrithi wa Mohamed Salah baada ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, kusisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza winga wao Michael Olise.

Liverpool ipo sokoni kusaka mchezaji wa kuziba pengo la Salah ambaye tayari ametangaza kuondoka mwishoni mwa msimu huu, huku Olise akiwa mmoja wa majina yaliyoingia kwenye rada ya klabu hiyo ya Anfield.

Ripoti kutoka Ulaya zinaeleza kuwa Liverpool iko tayari kuweka mezani dau kubwa la paundi 173 milioni (Sh594 bilioni) kwa ajili ya nyota huyo wa zamani wa Crystal Palace, huku pia Real Madrid wakitajwa kuwa tayari kutoa takribani paundi 143 milioni (Sh491 bilioni) kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.

Nyota wa Liverpool, Mohamed Sala ambaye ametangaza kuondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu. Picha na Mtandao

Hata hivyo, viongozi wa Bayern wameweka msimamo mkali kuwa Olise hauzwi kwa gharama yoyote kwa sasa. Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Max Eberl, amesisitiza kuwa hawafikirii hata kidogo kumuuza mchezaji huyo, akieleza kuwa bado ana kila kitu anachohitaji ndani ya Bayern.

Kwa upande wake, mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Jan-Christian Dreesen, ameongeza kuwa wachezaji wanaocheza Bayern wanaelewa thamani ya klabu hiyo, hivyo si rahisi kuwashawishi kuondoka.

Olise, mwenye umri wa miaka 24, ana mkataba wa miaka mitatu iliyobaki na hakuna kipengele cha kuvunjwa, hali inayofanya kuwa vigumu zaidi kwa klabu nyingine kumpata.

Winga wa Bayern Munich, Michael Olise anaripotiwa kupendekezwa kumrithi Mohamed Salah, lakini mabingwa hao wa Ujerumani wamesisitiza kutomwachia nyota huyo. Picha na Mtandao

Tangu ajiunge na Bayern mwaka 2024 kwa paundi 52 milioni (Sh180 bilioni), Olise amekuwa katika kiwango cha juu, akifunga mabao 16 na kutoa pasi za mabao 27 katika mechi 39 alizocheza msimu huu.

Wakati huohuo, Olise anatarajiwa kuwa na ratiba ngumu mbele yake, ikiwemo kukutana na Real Madrid katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kabla ya kuungana na timu ya taifa ya Ufaransa pamoja na nyota mwenzake Kylian Mbappe kuelekea mashindano makubwa yajayo.

Kwa sasa, inaonekana wazi kuwa Liverpool italazimika kutafuta mbadala mwingine wa Salah, kwani Bayern Munich wameweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuachia Olise kwa gharama yoyote katika dirisha lijalo la usajili.