Dondoo za mastaa wa Dabi

Hizi hapa ni baadhi ya dondoo za mastaa waliofanya vizuri hadi sasa kwenye ligi Kuu Bara na wanatarajiwa kuwemo kwenye mchezo wa leo wa dabi kati ya Yanga na Simba.


Stephane Aziz KI

Ndiye kinara wa mabao wa Ligi Kuu kwa sasa akiwa na mabao 14, lakini akiwa na asisti saba kwenye michezo ya ligi hadi sasa.


Yao Kouassi

Ndiye beki anayeongoza kwa asisti kati ya mabeki wote wa Ligi Kuu Bara msimu huu akiasisti mara saba.


Maxi  Nzengeli

Ndiye mchezaji pekee katika vikosi vya sasa aliyefunga mabao mawili katika mechi za Kariakoo Derby za Ligi.


Jonas Mkude

Ndiye mchezaji mwandamizi aliyecheza Kariakoo Derby nyingi kuliko wachezaji wote wa sasa wa timu hizo.


Clatous Chama

Kiungo mshambuliaji wa Simba anayeongoza kwa kuhusika na mabao mengi akifunga saba na kuasisti tano.


Kibu Denis

Ni kati ya wachezaji wenye mabao mengi katika derby za Ligi Kuu akifunga mawili sawa na Aziz KI na Maxi Nzegeli


Ayoub Lakred

Kipa huyo Mmorocco akianzishwa katika mchezo huo atakuwa ni wa kwanza kuikabili Yanga katika Ligi Kuu


Saido Ntibazonkiza

Ni kati ya wachezaji waliozichezea Simba na Yanga vipindi tofauti sawa na Jonas Mkude na Augustine Okrah ambao wanaweza kuwemo kwenye mchezo wa leo.