Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zitto: Mzee Sarungi asingekubali kuahirisha mechi ya Yanga, Simba

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga mwili wa Profesa Philemon Sarungi. Picha na Sunday George

Dar es Salam. Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kama Mzee Philimon Sarungi angekuwa hai, angekemea kwa ukali uamuzi wa kuahirisha mechi ya Dabi kati ya Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe Jumamosi Machi 8, katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam, akisisitiza uamuzi huo haukufaa kwa masilahi ya ligi ya Tanzania.

Zitto amesema kuwa Mzee Sarungi alikuwa ni shabiki mkubwa wa Simba na alijulikana kwa msimamo wake wa kutotaka kuona ligi ya Tanzania ikiporomoka au kupuuziliwa mbali na vilabu viwili tu vya Simba na Yanga.

"Sina hakika Mzee Sarungi angekuwepo juzi tulipotangaziwa kwamba mechi ya Dabi kati ya Simba na Yanga imeahirishwa angereact (angechukua hatua) namna gani, kwa sababu mzee alikuwa ni mnazi wa Simba kwelikweli, lakini naamini asingekubali upuuzi wowote ule wa kuifanya ligi yetu ionekane haina maana na inaendeshwa na vilabu viwili tu kati ya vilabu 16 vinavyoshiriki kwenye ligi," amesema Zitto.

Zitto ameyasema hayo leo, Jumatatu, Machi 10, 2025, katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, wakati wa kuaga mwili wa Profesa Sarungi aliyefariki dunia Machi 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam.


Endelea kufuatilia Mwananchi.