Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya mauaji ya katibu wa CCM Kilolo yapigwa kalenda

Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo wakitoka katika katika Mahakama  ya Wilaya ya Iringa. Picha na Mary Sanyiwa

Muktasari:

  • Kesi hiyo imeahirishwa leo Machi 3, 2025 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Rehema Mayagilo baada ya kusikiliza upande wa Jamhuri na utetezi

Iringa. Mahakama ya Wilaya ya Iringa imeahirisha tena kesi ya mauaji ya aliyekuwa katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kilolo, Christina Kibiki hadi Machi 10, 2025 itakapotajwa tena, huku sababu ikitajwa ni kutokamilika kwa upelelezi.

Kesi hiyo imeahirishwa leo Machi 3, 2025 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Rehema Mayagilo baada ya kusikiliza upande wa Jamhuri na utetezi.

Mawakili wa Serikali, Radhia Njovu na Cecilia Mrisho wameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria, upelelezi unapaswa kukamilika ndani ya siku 90 na kuiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi Machi 10, 2025.

Kesi hiyo kwa upande wa utetezi, inawakilishwa na Wakili Barnabas Nyalusi, Gloria Mwandelema na Neema Chacha ambao wameiomba Mahakama kukamilisha upelelezi mapema.

Baada ya kukamilika kwa usikilizwaji wa shauri hilo, watuhumiwa wote walirudishwa mahabusu hadi Machi 10, 2025 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Washtakiwa wa kesi hiyo ni Diwani wa Nyanzwa, Boniface Ugwale, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Kilolo, Hedikosi Kimwaga, Katibu wa Mbunge wa Kilolo, Kefa Walles, Silla Kimwaga na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mlandege, Wille Chikweo.

Watuhumiwa hao wote wanadaiwa kutenda kosa la mauaji Novemba 12, 2024 nyumbani kwa marehemu Kibiki, eneo la Banawanu, Kata ya Mseke mkoani Iringa.