Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampeni zapamba moto uchaguzi UWT

Muktasari:

Wakati leo Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) ikifanya uchaguzi wao ngazi ya Taifa, kampeni zimepamba moto nje ya ukumbi, wapambe wakitumia njia mbalimbali kuwanadi wagombea wao.

Dodoma. Kampeni za uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) zimepamba moto nje ya viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma huku wapambe wakitumia njia mbalimbali kuwanadi wagombea hao.

 Njia hizo ni pamoja na ngoma, matarumbeta, magari yaliyowekwa mabango na kupiga nyimbo zinazotaja majina ya wagombea na mabango yenye picha za wagombea.

Wapambe hao walifanya kampeni katika uwanja unaotumika kuegesha magari na hakuna watu walioruhusiwa kuingia kwenye geti la kuingilia katika ukumbi huo.

“Tutapekua hadi katika simu kama umeweka kipeperushi, hakikisha huingii ukumbini na kipeperushi,”amesikika mmoja wa walinzi wa chama hicho akiwaambia wajumbe wakati wa kuingia ukumbini.

Katika geti la kuingilia ukumbini, kulikuwa na vipeperushi vingi vilivyozagaa baada ya kutakiwa kutoingia navyo ndani.

Novemba 13, 2022, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyokutana Novemba 13, 2022 ilipitisha majina matano ya wagombea wa nafasi hiyo na majina manne ya nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa.

Majina yaliyopitishwa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni Gaudentia Kabaka anayetetea nafasi yake, Kate Kamba, Dk Wemael Chamshama, Mariam Lulinda na Mary Chatanda.

Mchuano mkali unaonekana kati ya Kabaka na Chatanda kwenye kampeni kubwa zinazofanyika katika viwanja hivyo,  mitandao ya jamii na barabara ya kuelekea ukumbini zikiwa zimepabwa na mabango ya wagombea hao.

Baadhi ya viongozi ambao washawasili katika ukumi huo ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa cha hicho, Daniel Chongolo na Naibu Katibu Mkuu Bara, Christine Mdeme.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan naye anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa uchaguzi.