Haya hapa matokeo ya ubunge CCM
Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) wameanza kutangaza matokeo ya kura za maoni za wagombea ubunge katika majimbo mbalimbali nchini, hatua muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Tanga
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Salehe Mhando ameongoza katika kura za maoni Jimbo la Kilindi, akipata kura 4,868 huku aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Omari Kigua akishika nafasi ya pili.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kilindi, Asha Mwendwe amesema wajumbe wote walikuwa 21,091 ambapo kura zilizopigwa ni 12,004 huku kura halali zikiwa 11,840 na zilizoharibika ni 168.
Amesema Kigua aliyeshika nafasi ya pili, amepata kura 2,516 ambapo amefuatiwa na Mohamed Mgati aliyepata kura 1,632. Wengine ni Seiya Keiya (1,262), Juma Kidunda (859) na Jabir Kigoda (703).
Aidha, Jimbo la Korogwe Mjini Charles Njama ameibuka mshindi kwa kupata kura 1,907 kati ya kura 3,100 zilizopigwa kwenye uchaguzi huo uliofanyika Agosti 4,2025.
Akitoa matokea ya uchaguzi huo, Katibu wa CCM Wilaya ya Korogwe, Evarist Mluge amesema kura halali ni 3,057 kati ya jumla ya 3,100 kura zilizopigwa ambapo kati ya hizo, 43 ziliharibika.
Ameongeza kuwa jumla ya wagombea kwenye uchaguzi wa Korogwe Mjini walikuwa saba ambapo mgombea nafasi ya pili alikuwa ni Dk Allen Kijazi aliyepata kura 573, akifuatiwa na Mathew Mganga (204), Thobias Nungu (175), Mhandisi Omari Zuberi (128) na Profesa Esther Dungumaro (45).
Kwa upande wa Jimbo la Handeni, Mhandishi Charles Sungura ameongoza kwenye kura za maoni katika jimbo hilo kwa kupata kura 2,510 kati ya kura zote halali zilizopigwa 11,247 huku myingine 204 zikiharibika.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Handeni, Mayasa Kimbau ametaja matokeo ya wagombea wengine kuwa ni Mhandisi Omari Chambo (1,056), Mussa Kidato (922), Abubakari Luchega (1,854), Athumani Malunda (624), Mhandisi Msafiri Mtemi (2,197), Yusuph Salimu (522) na Mhandisi John Sallu (1,358).
Charles Sungura aliongoza pia kwenye kura za maoni katika uchaguzi uliopita, hata hivyo aliyeshika nafasi ya nne John Sallu ndiye aliteuliwa na kamati kuu kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.
Kondoa Vijijini, Mjini
Mbunge aliyemaliza muda wake katika Jimbo la Kondoa Vijijini, Dk Ashatu Kijaji ameongoza kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo, akiwashinda wenzake wanne.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kondoa, Abdulrahim Hamidu amesema Dk Kijaji amepata kura 5,669 akifuatiwa na Hassan Lubuva aliyepata kura 3,593.
Wengine ni Said Mnyeke (577), Juma Shaban (84) na Hans Hida aliyepata kura 77.
Katika Jimbo la Kondoa Mjini, Mariam Ditopile ameongoza kura za maoni akipata kura 1,869 akimshinda mbunge aliyemaliza muda wake, Ally Makoa ambaye amepata kura 843.
Wengine ni Ally Juma (41) na Dk Athuman Mchana ambaye alipata kura saba.
Jimbo la Mpwapwa George Malima ametetea nafasi yake akipata kura 2,665. Malima ameongoza akimshinda mpinzani wake wa karibu, Njamasi Chiwanga aliyepata kura 2,140.
Kwenye matokeo hayo, Zakayo Mkemwa amepata kura 1,734, Juye Gussi (277), Adam Malima (257), Magreth Lema (178) na Exa Mpagama (104).
Ikungi Magharibi
Aliyekuwa mbunge wa Ikungi Magharibi, Elibariki Kingu amepenya kwenye kura za maoni za kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa kuongoza kwa kura 6,372 dhidi ya washindani wenzake watano.
Kwa matokeo hayo, Kingu anasubiri vikao vya uteuzi vingine vya Chama cha Mapinduzi ( CCM) vitakavyoketi kwa nyakati tofouti ili kutoa uamuzi wa mwisho.
Katika uchaguzi huo, Kingu amewashinda Shilinde Kasule aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,146, Ahmed Misanga kira 589, Hamis Mahuna kura 157, Mariam Nkumbi kundi 136 na Sauli Mndeme aliyeambulia kura 103.
Kibamba
Mshauri wa Rais, Angellah Kairuki ameibuka mshindi katika kura za maoni za ubunge za Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Kibamba akipata kura 4,655.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo, Henry Mwenge amesema Kairuki ameshinda kwa kupata kura 4,655 huku akimbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Issa Mtemvu aliyepata kura 615.
“Jumla ya kura zilizopigwa ni 5,696, kura zilizoharibika ni 45, kura halali 5,651,” amesema.
Wengine ni Nestory Yamungu aliyepata kura 76, Consolatha Rwiza (19), Angelo Nyonyi (43), Mwamini Mbwambo (64), Joseph Chikongoye (157) na Mchungaji Alphonce Temba (22).
Ludewa
Aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga ametetea nafasi yake baada ya kuongoza katika kura za maoni za kuwania ubunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.
Kamonga ametangazwa mshindi jana usiku Agosti 4,2025 baada ya pata kura 4,099.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Agosti 5, 2025 msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ludewa, Alfred Mwambeleko amewataja wagombea wengine na kura zao kuwa ni pamoja na Philipo Filikunjombe aliyepata kura 2,424, Merrion Ndofi kura 1,201, James Mkinga kura 139, Neema Mturo kura 67, Zephania Chaula kura 47 na Anumie Mtweve aliyeambulia kura 40.
"Matokeo haya ni hatua za awali, baada ya kamati kuu kukaa inaweza kuja na jina lolote kati ya haya, kwa hiyo wagombea wawe watulivu," amesema Mwambeleko.
Kakonko
Alan Mvano ameongoza katika matokeo ya kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kakonko akipata kura 1,453 huku mbunge aliyemaliza muda wake, Aloyce Kamamba akishika nafasi ya tatu
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Kakonko, Emmanuel Muhene, mgombea aliyeshika nafasi ya pili ni Emmanuel Gwegenyeza akipata kura 1,230 huku Kamamba akipata kura 509.
Wagombea wengine na kura walizopata ni Dk Pius Kagoma (491), Msakila Kabende (465), Modest Apolinary (319) na Rosemary Ruhinda (285).
Namtumbo
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Juma Homera ameongoza kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Namtumbo baaada ya kupata kura 11,836 kati ya kura 12,870 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia 92.
Akitangaza matokeo hayo, Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Namtumbo, Said Kusilawe amesema waliopiga kura kwenye uchaguzi huo ni 12,870 huku aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Vita Kawawa akishika nafasi ya pili kwa kura 852.
Wagombea wengine ni Mussa Chowo (327), Shaibu Majiwa (63) pamoja na Sharifu Ngonyani (182).
Korogwe Vijijini
Aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini, Timotheo Mnzava ameongoza kura za maoni katika uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika jana Jumatatu, Agosti 4, 2025 kwa kupata kura 8,522 huku mpinzani wake Dk Kalage John Petro akiambulia kura 1,572.
Katibu Wa CCM Wilaya Korogwe Vijijini, Safina Nchimbi aliyetangaza matokeo hayo amesema kura zilizopigwa zilikuwa 11,827, kura zilizoharibika 173 na kura halali zilikuwa 11,654.
Watiania wengine ni Mlewa Gabinus Gabriel 664, Prof Kinyashi George Frank 384, Magogo Amina Jumaa 301, Mohame Mwajuma Selemani 122, Mandia John Mtali 89, jumla ya Kura zilizopigwa 11,827, Kura, zilizoharibika 173.
Hanang
Aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Asia Halamga ameongoza katika kura za maoni za CCM Jimbo la Hanang kwa kupata kura 7,092, akiwaacha nyuma waliowahi kuwa wabunge katika jimbo hilo.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Neema Chuwa amesema mbali na Asia, Dk Mary Nagu, aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo, ameshika nafasi ya pili akipata kura 5,237.
Amesema mbunge aliyemaliza muda wake, Samwel Hhayuma ameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 2,995.
Wengine ni Franklin Sumaye aliyeshika nafasi ya nne kwa kura 399, John Lory (189) na Qambemeda Nyangura (152).
Makunduchi
Wanu Hafidh Ameir ameibuka mshindi katika kura za maoni nafasi ya ubunge wa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja kwa kupata kura 1,356 akiwazidi kwa mbali washindani wake wawili.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo, Othman Maulid Othman amemtaja aliyeshika nafasi ya pili ni Iddi Ali Moh’d ambaye amepata kura mbili na Pandu haji Yakoub aliyepata kura tatu.
Katika Bunge la 12 lililovunjwa Agosti 3, 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan, Wanu alikuwa mbunge wa viti maalumu na hivyo iwapo vikao vya chama ngazi ya juu vikimpitisha atakwenda kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Malinyi
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro, Antipas Mgungusi ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kupata kura (1,408), kati ya kura 5,269 zilizopigwa akitanguliwa na Dk Mecktrids Mdaku aliepata kura 2,450.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumanne, Agosti 5, 2025 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Nuru Ngereja, amesema wajumbe waliojitokeza kupiga kura walikuwa 5,286, kura 17 zimeharibika, halali 5,269. huku idadi ya wagombea wa nafasi hiyo ni Saba. Wagombea wengine ni DK. Florian Mballa (762), Hamidu Mwambungu (322), Deogratius Mbwasi (222), Zabron Mfungwasita (70) na Simon Ngonyani (70).
“Tumefanya zoezi hili kwa mafanikio makubwa, tunao wanachama wetu zaidi ya 70,000 ambao wamejitokeza katika zoezi la kura za maoni kwa mkoa wa Morogoro siku ya jana Julai 04, 2025. hawa ni wachache ambao wanafanya maamuzi kwa niaba ya wanachama wa chama cha Mapinduzi kwa Mkoa wa Morogoro zaidi ya 790,000," amesema Ngereja.
Chemba
Aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kunti Majala ameongoza kwenye kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Chemba.
Kunti alikuwa mmoja kati ya wabunge 19 wa viti maalumu kupitia Chadema ambao waliingia kwenye mgogoro na chama chao, lakini baada ya kuvunjwa kwa Bunge, aliibukia CCM na kuchukua fomu kutia nia kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Akitangaza matokeo katika uchaguzi huo, Katibu wa CCM Wilaya ya Chemba, Moza Abdallah amesema Majala amepata kura 5,809 akifuatiwa kwa mbali na Juma Nkamia aliyepata kura 1,220.
Wengine na kura zao katika mabano ni Amina Bakari (784), Omari Puto (408), Khamis Mkotya (196) na Francis Julius aliyepata kura 109.
Karagwe
Aliyekuwa Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa ameibuka kidedea katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) akipata kura 7,902 na kuwaacha mbali wapinzani wake watano.
Uchaguzi huo uliofanyika jana Agosti 4, 2025, Bashungwa amempiku mpinzani wake wa karibu, Confort Mugisha Blandes aliyepata kura 389.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Karagwe, Anatory Nshange, yanaonyesha wagombea wengine walivyopata kura kama ifuatavyo: Princepius Sabinian Rwazo (381), Akida Augustinio Mnyambo (113), Adolf Andrew Lwantungamo (110) na Devotha Obadia Alexanda (13).
Nshange amesema jumla ya wajumbe 8,969 walipiga kura ambapo kura halali zilikuwa 8,908 na kura 61 ziliharibika.
Babati Mjini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Emmanuel Khambay ameongoza kwenye kura za maoni ya ubunge katika jimbo hilo akipata kura 2,487.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Babati, Mohamed Chollaje amesema Khambay ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia wilaya hiyo, ameongoza uchaguzi huo uliohusisha wagombea saba.
Amesema aliyeshika nafasi ya pili ni Hindi Mastahi akipata kura 439, akifuatiwa na Joanes Darabe (374) na Flora Hondi (175). Wengine ni Sofia Kwang’ (146), Patrice Gwasima (53) na Peter Salanga (38).
Temeke
Kisangi wa Jimbo la Temeke, Abdallah Chaurembo wa Chamazi na Kakulu Kakulu wa Mbagala wametangazwa kuongoza kura za maoni katika Majimbo matatu yaliyopo wilaya ya Temeke.
Watia nia hao katika Jimbo la Temeke wametangazwa leo Agosti 5,2025 saa 11 alfajiri na Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke Daniel Sayi.
Akitangaza matokeo ya Jimbo la Temeke, Sayi amesema watia nia nane walishiriki ambapo Jasdeep Singh amepata kura 959 sawa na asilimia 14, Shafi Dauda 887 sawa na asilimia 13, Dorothy Kilave 288 sawa na asilimia nne, Fadhili Mohamed 1,389 sawa na asilimia 21, Mariam Kisangi 2,367 sawa na asilimia 55, Mussa Mtulya 60 sawa na asilimia moja, Bernard Mwakyembe 769 sawa na asilimia 11, Leah Mwampishi 48 sawa na asilimia moja.
Kwa Jimbo la Chamazi wagombea walikuwa saba ambapo Munir Adam 19, Hamidu Bobali 56, Abdallah Chaurembo 2,765 sawa na asilimia 82, Meleckzedeck Hango 391, Mariam Kambi 30, Mohamed Rajabu kura tano na Zuhura Mazrui kura 12.
Jimbo la Mbagala lililokuwa na wagombea saba David Fumbuka kura 49 sawa na asilimia moja, Kakulu Kakulu 2,364 sawa na asilimia 47, Issa Mangungu kura 795 asilimia 16, Judith Mollel 25 sawa na asilimia moja, Abdallah Mtinika 760 sawa na asilimia 15, Dk Elisha Osati kura 450 sawa na asilimia tisa, Seif Sulle 553.
Peramiho
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama ameshinda kura za maoni za Chama cha mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo akipata kura 7,167 kati ya kura 8,575, akiwaacha kwa mbali washindani wake.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Juma Nambaira amesema waliopiga kura ni 8,575 ambapo Jenista ameongoza kwa kura 7,167.
Wagombea wengine na kura walizopata ni: Godfrey Tindwa (0), Justine Njelekela (1), Hamdan Hamdan (2) na Jenista Mhagama (7,167).
Mkuranga
Aliyekuwa mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, Abdallah Ulega ameongoza kura za maoni jimboni humo baada kuwashinda wapinzani wake wanne katika mchakato huo.
Ulega ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, amepata kura 8490, dhidi ya Mohamed Kilolile aliyepata 4,293, Gift Mipiko kapata 440, Mwasiti Matola amepata kura 170 na Prisca kaambulia kura Ngwashemi 22.
Taarifa za matokeo hayo zinaeleza kuwa jumla ya wapigakura ni 1,3398.
Rufiji
Mohamed Mchengerwa ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kura za maoni za ubunge wa Rufiji kwa kupata kura 8,465 sawa na asilimia 99.19 ya kura zote 8,533 zilizopigwa huku kura moja ikiharibika.
Mchengerwa aliyekuwa akichuana na wenzake watatu, amewaacha kwa mbali huku aliyemfuatia, Salima Ponga akipata kura 34, Selemani Mhekela kura 26 na Hamisa Kisoma kura nane.
Mtia nia huyo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ametetea nafasi hiyo ya ubunge kwa miaka kumi nyuma na sasa anasubiri uamuzi wa vikao vya juu.
Vwawa
Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Vwawa, Japhet Hasunga ameongoza kura za maoni katika jimbo hilo kwa kupata kura 5,604.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Vwawa, Halima Yusuph ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu Mkoa wa Songwe amesema Hasunga ameongoza kwa kupata kura 5,604 akifuatiwa na Tiksoni Nzunda aliyepata kura 1,451.
Halima amewataja wengine kuwa ni Fanuel Mkisi (820), Godfrey Mwashitete (392), Happy Mgala(259) na Jumanne Sichizya(229).
Amesema hizi ni kura za awali za maoni kwani bado mchakato wa vikao vya ndani unaendelea kwa ajili ya kuteua jina moja Kati ya hawa waliopigiwa kura, hivyo amewaomba wawe watulivu.
Serengeti
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mara, Mary Daniel ameongoza kwenye kura za maoni katika Jimbo la Serengeti, huku akimshinda kwa mbali Dk Stephen Kebwe.
Katika kinyang'anyiro hicho mbunge aliyemaliza muda wake, Amsabi Mrimi naye hakuweza kufurukuta baada ya kushika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo uliohusisha wagombea sita.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Serengeti, Abubakar Ghati amesema Mary ameongoza kwa kupata kura 11,533 akifuatiwa na Dk Kebwe aliyepata kura 2,903.
Katika uchaguzi huo Amsabi Mrimi amepata kura 1,400, Michael Mahende amepata kura 1,029, Paulo Chacha akipata kura 213 na Deogratias Chacha akipata kura 489.
"Wagombea walikuwa sita, kura zilizopigwa ni 17,981 ,kura zilizoharibika ni 413 na kura halali zilikuwa ni 17,568," amesema Ghati.
Monduli
Mbunge aliyemaliza muda wake katika Jimbo la Monduli mkoani Arusha, Fredrick Lowassa ameongoza kwenye uchaguzi wa kura za maoni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jana.
Lowassa ambaye amewania muhula wake wa pili amepata kura 7,137 akimwacha mshindani wake wa karibu,Isack Joseph, maarufu 'Kadogoo' aliyekua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli katika Baraza la madiwani lililomaliza muda wake kwa kura 2,206.
Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Rukia Mbasha alisema wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni Wilson Kurambe (952),Shabani Adam (251),Bilihuda Kisaka (41) na Sakaya Alaisheri (21).
Mbasha amesema kura zilizotarajiwa kupigwa ni 12,950 wakati waliopiga kura ni 10,745 kura zilizoharibika 137 na kura halali zilikua 10,608.
Longido, Karatu
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa, ameongoza kura za maoni katika Jimbo la Longido kwa kupata kura 9,054.
Aidha katika jimbo la Karatu, Mbunge aliyemaliza muda wake, Daniel Awack ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 7,884, akiwashinda wagombea wenzake wanne akiwemo aliyekuwa mbunge wa viti maalumu Chadema,Cecilia Pareso.
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM Wilaya ya Longido,Geofrey Kavenga alisema idadi ya wajumbe ilikuwa 12,782 kati ya hao waliopiga kura ni 11,759 na zilizoharibika ni kura 59.
Alisema wagombea wengine na idadi ya kura zao kwenye mabano ni Petro Ngarikoni (1,421), Nicholous Senteu (1,128) na Martha Ntopo (87).
Kwa upande wa jimbo la Karatu,Katibu wa CCM wilaya ya Karatu,Hanafi Msabaha alisema aliyepata nafasi ya pili ni Cecilia Paresso aliyepata kura 1,341.
Wengine na idadi ya kura zao kwenye mabano ni Patrice Mattay (658), Pantaleo Paresso (142) na Shedrack Qamna (55).
Kwa mujibu wa Katibu huyo idadi ya wajumbe ni 12,285 waliopiga kura ni 10,384. halali zilikuwa 10,080 na zilizoharibika ni 156.
Arumeru Mashariki
Matokeo ya kura za maoni za Ubunge Arumeru Mashariki zimemwendea vyema Joshua Nassari kwa kupata kura 6,678.
Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Rehema Ndele amesema Dk John Pallangyo aliyekuwa akitetea nafasi hiyo amepata kura 652, Elisa Mbisse kura 650, Profesa Daniel Pallangyo 372, Johnson Sarakikya 312, William Sarakikya 307, Anjela Pallangyo 105 na Rose Urioh 55.
Nassari aliwahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chadema baadaye akahamia CCM.
Uzini
Aliyekuwa Naibu Waziri Muungano na Mazingira, Hamza Chilo ameangushwa katika kura za maoni Jimbo la Uzini.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi, Rajab Ali Rajab amesema Chilo amepata kura 395 akitanguliwa na Ali Mdowe aliyepata kura 915 na kuibuka kidedea.
Kwa nafasi ya uwakilishi Abdalla Msigiri ameibuka kidedea kwa kupata kura 555 akifuatiwa na Salum Ali Haji kura 421 huku Salum Ramadhan Abdallah akipata kura 238.
Rorya
Mbunge aliyemaliza muda wake katika Jimbo la Rorya Mkoa wa Mara, Jafari Chege ameongoza katika kura za maoni kwenye jimbo hilo baada ya kupata kura 7,866.
Chege amewashinda makada wenzake wanne aliokuwa akigombea nao kwenye kinyang'anyiro hicho kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini kote jana Agosti 4, 2025.
Katibu wa CCM Wilaya ya Rorya, Hassan Moshi amesema nafasi ya pili imekwenda kwa Sango Kasera aliyepata kura 4,785 huku Nyihita Wilfred akishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 1,034.
Nchama Wambura amekuwa wa nne katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 380 huku nafasi ya tano ikienda kwa Peter Sarungi aliyepata kura 183.
Sintofahamu Mfenesini
Matokeo ya kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mfenesini mjini hapa yamechelewa kutangazwa kutokana na sintofahamu iliyojitokeza kutokana na kura kudaiwa kuongezeka.
Idadi ya wajumbe walikuwa 472 lakini baada ya kura kuhesabiwa zikafikia 528, sawa na ongezeko la kura 56.
Baada ya kuibuka changamoto hiyo, Katibu wa Wilaya Mfenesini, Veronica Ndaro ameagiza kura zote zipelekwe wilayani ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo kwa ngazi za juu.
Awali, uchaguzi huo ulikuwa na sintofahamu kwa baadhi ya wajumbe waliokuwa wamevaa sare za chama zenye nembo badala ya zinazotakiwa.
Chamwino
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Deogratius Ndejembi ameibuka kinara katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura (8,655) huku mpinzani wake wa karibu, Joel Mwaka, akipata kura (117).
Matokeo hayo yametangazwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Chamwino, Ibrahim Mpwapwa, baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa jimbo hilo kupiga kura.
Mbinga
Aliyekuwa mbunge katika Jimbo la Mbinga Mjini, Jonas Mbunda ameibuka kidedea kwenye kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo, akipata kura 5,826 kati ya kura 7,289 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga, Ally Simba amesema waliopiga kura walikuwa 8,579 lakini kura halali zilikuwa 7,289.
Simba ametaja matokeo ya wagombea wengine kama ifuatavyo: Frank Ndunguru (277), Dk Noel Komba (1,417) na Jonas Mbunda (5,826).
Lupa
Aliyekuwa Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka ameibuka kidedea kwenye kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Lupa akipata kura 5,572 huku akiwaacha mbali washindani wake.
Masache amepata ushindi huo dhidi ya washindani wake watatu akiwamo Noel Ntangu aliyepata kura 2,821, Geoffrey Mwankenja (2,115) na Sarah Sampo (143).
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chunya, Charles Jockel amelieleza Mwananchi kwamba uchaguzi huo umekwenda vizuri katika kata zote 10 zilizopo katika jimbo hilo.
Sura mpya Geita, katoro
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Constantine Kanyasu na Tumaini Magesa wa Jimbo la Katoro, wameshindwa kuchomoza kwenye kura za maoni za kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 kupitia Chama chao cha Mapinduzi (CCM).
Kanyasu ambaye amehudumu kama Mbunge wa Geita Mjini kwa kipindi cha miaka 10, amejikuta akipata kura 2,097 huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Chacha Wambura aliyepata kura 2,145.
Chacha Wambura
Wengine waliofuatia ni Upendo Peneza kura 1,272, Gabriel Luhumbi kura 119 na John Saulo kura 36.
Kwa upande wa Tumaini Magesa, aliyekuwa Mbunge wa Busanda kwa miaka mitano na mwaka huu akaamua kuwania Jimbo jipya la Katoro, ameshika nafasi ya tatu katika mbio hizo baada ya kupata kura 1,265.
Katika Jimbo hilo, Kija Ntemi ameongoza kwa kupata kura 2,134 akifuatiwa na Ester James aliyepata kura 2,075, huku wagombea wengine wakiwa ni Simon Marando aliyepata kura 549 na Mathias Lupuga kura 232.
Akitangaza matokeo hayo usiku huu, msimamizi wa uchaguzi huo, Michael Msuya ambaye amesimamia majimbo manne ya Wilaya ya Geita, amesema jumla ya wapiga kura waliotarajiwa ilikuwa ni 6,588.
Kura zilizopigwa ni 5,726, kati ya hizo, kura 57 zimeharibika na kura halali zilikuwa 5,682.
Katika Jimbo la Geita, Mbunge aliyemaliza muda wake, Musukuma Kasheku ameibuka kinara kwa kupata kura 5,251, akifuatiwa na Emanuel Luponya kura 1,997, Patric Stephen kura 381 na Sophia Mashala kura 44.
Kwa upande wa Jimbo la Busanda lenye kata 11, Dk Jafar Seif ameongoza kwa kupata kura 5,286.
Waliomfuatia ni Lorencia Bukwimba kura 927, Dk Busanda Lucas kura 392 na Dk Salum Mathias kura 23].
Katika jimbo hilo, kura zilizopigwa zilikuwa 6,909, huku kura 108 zikiharibika na kura halali zilikuwa 6,783.
Same Mashariki
Mbunge wa Same Mashariki aliyemaliza muda wake, Anne Kilango ameongeza kurs zs msoni katika jimbo hilo kwa kupata kura 3, 029 kati ya kura 5 395 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Same Mashariki, Amos Kusakula amesema Kilango ameongeza kwa kupata kura 3,029 akifuatiwa na Miryam Mjema aliyepata kura 1,763.
Wengine ni Andrea Chezue aliyepata kura (358), Adam Mzee(60), Daud Mambo(51), Nickson Mjema (45) na Dk Peter Kibacha(24).
Amesema idadi ya wajumbe waliopiga kura ni 5 395, kura zilizoharibika ni 65 na kura halali ni 5,330.
Same Magharibi
Mbunge wa Same Magharibi aliyemaliza muda wake, Dk Mathayo David ameongeza kura za maoni za ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 5,093 kati ya kura 7, 323 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo usiku huu wa kumakia leo Jumanne Agosti 5, 2025, Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Amos Kusakula amesema Dk David ameongeza kwa kupata kura 5,093 na kufuatiwa na Fatuma Kange aliyepata kura 875.
Wengine ni Profesa Ladslaus Mnyone (721), Philemon Mchome (272), Niwaheri Mndeme (150), Yusto Mapande (77) na Goodluck Mchome (51).
Aidha, amesema idadi ya kura zilizopigwa ni 7,323, huku zilizoharibika ni 84 na halali ni 7,239.
Bukoba Vijijini
Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Bukoba Vijijini kimetangaza matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni ya wabunge wa Jimbo hilo ambapo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dk Jasson Rweikiza ameongoza kwa kupata kura 6,465 huku mgombea mwenzake aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM, mkoani Kagera, Faris Buruhan akifuatia kwa kupata kura 4,619.
Akitangaza matokeo ya kura hizo usiku huu wa kuamkia Jumanne Agosti 5,2025 katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera, Jesca Ndyamkama amesema kura zilizopigwa ni 11,682 na kura 100 zimeharibika.
Amewataja wagombea wengine ni Fahami Juma (239),Asted Mpita (124),Edmundi Rutaraka (89),na Philebart Bagenda (44).
Faris, baada ya kutangazwa matokeo hayo amepata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari huku akitaja kutoridhishwa na matokeo hayo na kusema yaligubikwa na vitendo vya rushwa jambo lilompelekea kutosaini fomu za kukubaliana na matokeo, akisema kuwa tayari ameanza hatua za kupeleka malalamiko kwenye chama ngazi ya mkoa.
Nyamagana
Mwanza. Mbunge anayetetea nafasi yake katika Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula ameibuka kidedea kwenye kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 3,711.
Akitangaza matokeo hayo usiku huu katika ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana, Katibu wa chama hicho, Deogratias Nakey amesema anayefuatia ni John Nzilanyingi aliyepata kura 1,811.
Wagombea wengine na kura walizopata kwenye mabano ni Laurence Masha (746), Dk Phillip Makoye (530), Pendo Costantine (86), Henry Chotta (42), na Erick Gwaje (19).
Hata hivyo, Nakey amesisitiza kuwa kuongoza katika kura za maoni hakumaanishi mgombea amepitishwa rasmi kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu.
“Kuongoza kwa kura siyo kwamba tayari ameteuliwa. Tutasubiri vikao vya uteuzi vya Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu,” amesema Nakey.
Morogoro Mjini
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro kimetangaza matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni ya wabunge wa Jimbo hilo na AbdulAziz Abood ameongoza kwa kupata kura 4,511 huku mgombea Ally Simba akipata kura 1,886.
Akitangaza matokeo ya kura hizo usiku huu, Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro, Twalib Bellege amewataja wagombea wengine kuwa ni Robert Kadikilo aliyepata kura 131, Bupe Kamugisha kura 60 na Tecra Mbiki amepata kura 46.
Wengine ni Halfani Makila aliyepata kura 28 na Tito Mlelwa ameambulia kura 13 huku kura zilizopigwa jumla yake ikiwa ni 6,485, zilizoharibika ni 84 na kura halali zikiwa 6,401.
Tabora Mjini
Shabani Mruthu ameibuka mshindi katika kura ya maoni ndani ya CCM baada ya kupata kura 6,612 kati ya kura halali 7,763 zilizopigwa katika Jimbo la Tabora Mjini.
Mruthu alikuwa akishindana na watia nia wengine watano akiwamo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga
Katika kinyang’anyiro hicho, Mwaifunga amepata jumla ya kura 326 na kushika nafasi ya tatu.
Matokeo hayo yametangazwa usiku huu na Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora, Daniel Mhina aliyebainisha kuwa jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 7,882, huku kura 119 zikiharibika.
Wagombea wengine akiwamo Kisamba Tambwe amepata kura 395, Emmanuel Mwakasaka kura 228, Godbless Mafole kura109 na Deusdedith Kanunu kura 93. Akizungumza baada ya matokeo kutangazwa, Mwaifunga amesema; “Ninaendelea kujifunza taratibu na mifumo ya CCM. Mimi bado ni mpya katika chama hiki na naamini kila hatua ni sehemu ya safari ya siasa.”
Kwa upande wake, mshindi wa kura hizo, Shabani Mruthu, amesema endapo atateuliwa rasmi kuwa mgombea, ataendeleza heshima ya chama hicho kwa kufanya kazi kwa bidii na uaminifu kwa wananchi wa Tabora Mjini.
Kinondoni
Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba ameongoza kura za maoni za ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwashinda wenzake saba akiwemo mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Idd Azzan.
Wakati Tarimba akiibuka kidedea Kinondoni, naye Geofrey Timothy ameongeza kura za maoni katika jimbo la Kawe ambalo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Askofu Josephat Gwajima hakujitokeza kutetea nafasi hiyo kwa muhula mwingine.
Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia Jumanne Agosti 5,2025 msimamizi wa uchaguzi huo, Jacob Siayi amesema Tarimba amepata kura 2, 646 akiwashinda Wilfred Nyamwija (1,271) Idd Azzan ( 484) Michael Wambura ( 84) Jerusa Kitoto( 24) Zena Kiputiputi ( 14) Julieth Rushuli ( 7) na Wangota Salum ( 3).
Kwa mujibu Siayi, jumla za kura zote zilizopigwa katika Jimbo la Kinondoni 4,553.
Katika Jimbo Kawe Siayi amesema Timothy ameongoza kwa kura 3,657 Leonard Manyama ( 953) Maria Sebastian (775),Philip Matondo (176) Elias Komba(158), Hemed Nkunya (147) Godwin Kamala ( 112) na Derek Murusuri( 63) .
Shinyanga mjini
Mkurugenzi wa uchaguzi Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni katibu wa CCM wilaya, Halima Chacha amemtangaza Patrobas Katambi kuwa mshindi wa kura za maoni huku akiwataka wagombea kuungana kwa pamoja na kukilinda chama, kwa sababu mchakato wa uchaguzi bado unaendelea kumchagua mgombea mmoja wa jimbo.
Akizungumza leo baada ya majumuisho ya kura za maoni kutoka kata 17 na kutangaza matokeo na kuongeza kuwa hata kama mtu kapata kura chache za maoni huu sio mwisho.
“Patrobas Katambi ameongoza kwa kura 2,920 akifuatiwa na Steven Masele kura 874, Paul Ndanji (34) Abbubakar Mukadam 25, Athumani Fatihu (17), Hosea Karume (16) na Astati Ngatale (10)” amesema Halima.
Iringa Mjini
Fadhili Ngajilo ameongoza kura za maoni katika uchaguzi wa CCM uliokamilika usiku huu baada ya kupata jumla ya kura 1,899 huku anayemfuatia, Moses Ambindwile akijipatia kura 1,523.
Matokeo hayo yametangazwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa, Hassan Makoba katika ofisi za CCM wilaya zilizopo Sabasaba Kata ya Gangilonga, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Akiendelea kutangaza matokeo hayo Katibu Makoba amemtanngaza Jesca Msambatavangu mbunge aliyemaliza muda wake wa ubunge kuwa amepata kura 408 huku Peter Msigwa akijipatia 477, Edward Chengula 188 na Islam Huwel kura 136.
Makoba amewaomba wagombea wote kuwa; "Haya ni matokeo ya kuongoza kura za maoni hivyo niwaombe muwe watulivu tusubiri uamuzi wa vikao vingine vya chama.
Kikwajuni
Wakati mbunge anayemaliza muda wake Jimbo la Kikwajuni, Hamad Masauni akiibuka kidedea katika kura za maoni, mwakilishi anayemaliza muda wake Nassor Salim Ali ameangushwa.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Rukia Omar, Masauni ambaye pia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira amepata kura 790 kati ya kura 954 zilizopigwa na zilizoharibika ni 13.
Masauni amefuatiwa kwa ukaribu na Said Ali Karume aliyepata kura 50.
"Hamid Abdala Hamid amepata kura 36, Farnahidi Sultan na Malik amepata kura 35,"
Maua Abdalla amepata kura 27 na Khadija Seif Salum akiambilia kura tatu.
Uwakilishi
Katika nafasi ya uwakilishi Fuad Shaib Ahmada amepata kura 286 na kumwangusha aliyekuwa anatetea nafasi hiyo Nassor Salim Ali aliyepata kura 192 kati ya kura 954 zilizopigwa.
Msimamizi amesema kura 14 zimeharibika. Wengine ni Abdala Ibrahim Natepe amepata kura 180, Asha Nassib Salim akipata kura 40 na Victor Lazalo akipata kura 14.
Pangani
Aliyekuwa Mbunge wa Pangani, Mkoa wa Tanga, Jumaa Aweso ameongoza kwenye kura za maoni kwa kupata asilimia 100 ya kura zote 3,806 zilizopigwa katika kata 14 za jimbo hilo.
Aliyekuwa Mbunge wa Pangani, Mkoa wa Tanga, Jumaa Aweso
Akizungumza na Mwananchi, kuhusu matokeo hayo Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Pangani, Abdul Swala amesema katika kata zote za jimbo hilo Aweso ameongoza kwa kura huku wagombea wenzake wakipata sifuri, hivyo kuibuka mshindi.
Mbali na Aweso, wengine ni Mariam Abdallah na Ramadhan Zuberi.
Amesema katika uchaguzi huo wajumbe wote ni 3,843 ambao walitakiwa kupiga kura, lakini 37 hawakufika kwenye vituo vya kupigia kura na kufanya jumla ya kura zilizopigwa kuwa 3,806 ambapo hakuna iliyoharibika.
Baada ya matokeo hayo, Aweso anayetetea jimbo hilo kwa kipindi cha tatu ambaye pia ni Waziri wa Maji ametumia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram kushukuru kwa kuandika: Asanteni sana wajumbe wa CCM Jimbo la Pangani kwa kura zote za ndio. Imani hii mlionipa nitailipa kwa matendo."
Bukombe
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Dk Dotto Biteko ameibuka mshindi wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata asilimia 99.8 ya kura zilizopigwa.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dk Doto Biteko.
Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu, Katibu wa CCM Jimbo la Bukombe, Mwakalukwa Leonard, amesema jumla ya wajumbe 7,456 walishiriki kupiga kura ambapo kura halali zilikuwa 7,441 huku kura 15 pekee zikiharibika.
“Kura zote 7,456 zilipigwa, hakuna kura ya hapana, kura 15 zimeharibika,"amesema
Biteko alikuwa mgombea pekee katika nafasi ya ubunge kwa Jimbo la Bukombe katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.
Arusha Mjini
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameongoza kura za maoni katika nafasi ya ubunge Jimbo la Arusha Mjini kwa kupata kura 9,056.
Makonda na wenzake sita walikuwa wakiwania nafasi kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM), katika jimbo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na Mrisho Gambo.
Matokeo hayo yametangazwa leo na Mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Timothy Sanga amesema jumla ya wajumbe ilikuwa ni 10,186 ila waliopiga kura ni 9,276.
Wengine na matokeo yao kwenye mabano ni Mustapha Nassoro (83),Hussein Gonga (46),Ally Babu (28),Aminatha Toure (26),Lwembo Mghweno (16) na Jasper Kishumbua (10).
Songea Mjini
Aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Dk Damas Ndumbaro ameongoza kura za maoni katika nafasi ya ubunge Jimbo la Songea Mjini kwa kupata kura 3,391 kati ya kura 6,795 zilizopigwa.
Aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Dk Damas Ndumbaro
Dk Ndumbaro na wenzake wanne, walikuwa wakiwania nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Songea Mjini kwenye uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025. Ndumbaru anatetea kiti hicho.
Akitangaza matokeo hayo leo, Mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Songea, James Mgego amesema jimbo hilo lina jumla ya kata 21 kura halali zilizopigwa ni 6,736 na zilizoharibika ni 59.
Amemtaja aliyeshika nafasi ya pili ni Hemed Challe aliyepata kura 2,839, Amandus Tembo kura 279, Issa Mkwawa kura 143 na Regan Mbawala kura 84.
Hata hivyo, msimamizi huyo amesema kura zilizopigwa leo ni za maoni, mchakato bado unaendelea. “Kwa hiyo wagombea wote muendelee kuwa watulivu kama tulivyofanya leo, uchaguzi umekuwa wa haki na amani imetawala,” amesema Mgego.
Moshi Mjini
Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo ameongoza kura za maoni katika jimbo hilo kwa kupata kura 1,539 kati ya 3,298 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi, Ivan Moshi ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro amemtangaza Priscus kuongoza kwa kura akifuatiwa na Ibrahim Shayo aliyepata kura 1,495.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo, Moshi amesema kura zilizopigwa zilikuwa 3,298, kura zilizoharibika ni 10 na halali zikiwa ni kura 3,288.
Amesema wagombea wengine ni Amin Twaha (143) Samwel Ngowi (67), Theresia Komba (36) na Profesa Neema Kumburu (8). Aidha Moshi amesema hayo ni matokeo ya awali na kwamba vikao vya chama bado vinaendelea.
Ubunge Misenyi
Aliyekuwa mbunge wa Missenyi mkoani Kagera, Florente Kyombo ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 2,979 kati ya 5,919 zilizopigwa katika vituo 22 za jimbo hilo.
Msimamizi wa uchaguzi wa Chama cha mapinduzi (CCM), Bakari Mwacha amesema kati ya wajumbe 5,919 waliotakiwa kupiga kura, 5,124 ndiyo walipiga kwenye vituo vyote.
Aliyekuwa mbunge wa Missenyi mkoani Kagera, Florente Kyombo
Mwacha amemtaja Kyombo anayeomba ridhaa ya kutetea nafasi hiyo kwa kupata kura 2,979 akifuatiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya, Projestus Tegamaisho aliyepata 1,355.
Wengine na kura zao kwenye mabano ni, Assumpter Mshama (475), Pelacius Ndibalema (166), Naswiru Byabatokura (88), Jacklyne Rushaigo (52), Jacklyne Rushaigo (52) na Amina Athuman kura tisa.
Musoma Mjini
Mgore Miraji ameibuka mshindi kwenye kura za maoni baada ya kuwabwaga wapinzani wake watano aliokuwa akishindana nao katika mchakato wa kumpata mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu ujao katika Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara.
Endapo Mgore atapitishwa na kamati Kuu ya chama chake kupeperusha bendera na kisha kuwa mshindi katika uchaguzi huo, basi atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa mbunge wa jimbo hilo la Musoma Mjini.
Mgore Miraji ambaye ameongoza kura za maoni ubunge Musoma Mjini
Akitangaza matokeo ya kura za maoni kwa Wilaya ya Musoma Mjini, Katibu wa CCM wilayani humo, Burhan Ruta amesema Mgore amepata kura 2,255 huku mpinzani wake wa karibu Juma Mokili akipata kura 1,543.
Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni pamoja na Dk Eliud Esseko (115), John Bwana (43), Philbert Sasita (34) na Mashaka Biswalo (44).
“Jumla ya kura zilizopigwa ni 3,796, zilizoharibika ni 62 na halali zilikuwa 3,734, kwa hiyo namtangaza Mgore kuwa ameongeza kwenye kura za maoni,” amesema.
Ruta amesema kutokana na kanuni za chama hicho, mgombea aliyeongoza katika kura za maoni hapaswi kufanya sherehe ya aina yoyote kabla ya vikao vya uteuzi kwa maelezo kuwa kuongoza sio kigezo cha kuteuliwa na chama.
Bukoba Mjini
Mhandisi Johnston Mtasingwa ameongoza kwenye kura za maoni kusaka uteuzi wa kuwania ubunge katika Jimbo la Bukoba Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Katika uchaguzi huo uliofanyika leo 2025 Mhandisi Mtasingwa ameongoza kwa kupata kura 1,408 kati ya kura halisi zilizopigwa 2,958.
Mhandisi Johnston Mtasingwa
Wengine waliomfuatia kwenye uchaguzi huo ni Alex Denis (804), Almasoud Kalumuna (640), Jamila Hassan (66) na Koku Rutha (44).
Makambako
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ameshinda kura za maoni katika Jimbo la Makambako mkoani Njombe akimshinda mpinzani wake, Deo Sanga.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo.
Chongolo ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametangazwa mshindi kwa kupata kura 6,151 kati ya 6,624.
Sanga maarufu kama Jah People ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 470.
Rombo
Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Rombo, ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 5,125 kati ya 6,156 zilizopigwa.
Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Rombo, ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda.
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Mossoud Melimeli amemtangaza Profesa Mkenda kuwa mshindi akifuatiwa na Antony Mseke aliyepata kura 824.
Wagombea wengine katika uchaguzi huo ni Samora Kanje (64), Jackline Silemu (61) na John Nicholous (32).
Ngara
Mkuu wa vipindi Clouds TV, Dotto Bahemu ameongoza kura za maoni katika nafasi ya ubunge jimbo la Ngara akipata kura 6,855 kati ya kura 9,705 zilizopigwa.
Bahemu amepata kura 6,855 akifuatiwa na Stephen Kagaigai aliyepata kura kura 2,344.
Matokeo hayo yametangazwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ngara, Mariam Amiri ambaye amesema wapiga kura walikuwa 12,000 lakini waliopiga kura ni 9,705 na kura iliyoharibika ni moja tu.
Ilala
Aliyekuwa mbunge wa Ilala na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameongoza kura za maoni katika nafasi ya ubunge Jimbo la Ilala kwa kupata kura 2,485 kati ya kura 2,822 zilizopigwa.
Zungu na wenzake sita, walikuwa wakiwania nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam kwenye uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Mchakato huo wa upigaji kura za maoni umefanyika leo Agosti4,2025.
Akitangaza matokeo hayo leo saa 3:40 usiku, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Chief Sylvester Yeredi amesema aliyeshika nafasi ya pili katika mchakato huo ni Mendrad Mpangala aliyepata kura 139 akifuatiwa na Grace Buberwa aliyepata kura 106.
"Stella Njau amepata kura nane, Isack Kitogo 35 na Rose Bisenddo wamegawana kura zilizobaki,"amesema.
Nyassa
Aliyekua Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, John Nchimbi ameongoza kura za maoni Jimbo la Nyasa baada ya kupata kura 9,157 kati ya kura 10,695 zilizopigwa akifuatiwa kwa mbali na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Stellah Manyanya aliyepata kura (548).
Segerea
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonna Kamoli ameibuka kinara kwenye kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akipata kura 4,510 akifuatiwa na Rajab Abdallah aliyepata kura 1,756.
Wengine ni Aidan Kwezi aliyepata kura 272, Kassim Nyihuka amepata kura 205, Gidion Mandes aliyepata kura 154, Abdallah Mashausi akipata kura 93, na Nyimadi Yange akipata kura 52.
Ukonga
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa ameibuka kinara kwenye kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambapo ameongoza kwa kura 2,332 aifuatiwa na Rajab Nyangasa akipata kura 624, Rangi Nyoma (128), Mndele amepata (112), na Alawi Rwegoshora amepata kura 195.
Akitangaza matokeo hayo leo Katibu wa CCM, Wilaya ya Ilala, Chief Sylivester kabla ya kutoa majumuisho, amesema matokeo hayo ni maoni ya wanachama lakini vikao vinaweza kuamua vinginevyo.
Vunjo
Enock Koola ameongoza kura za maoni katika Jimbo la Vunjo, Wilaya ya Moshi kwa kupata kura 1,999 na kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk Charles Kimei aliyepata kura 861.
Akitangaza matokeo hayo leo Agosti 4, 2025 Msimamizi wa uchaguzi huo, Ramadhani Mahanyu ambaye pia ni katibu wa CCM Moshi Vijijini, amesema kura zilizopigwa ni 4,080, zilizoharibika 26 huku halali zikiwa kura 4,054.
Amewatangaza wagombea wengine kuwa ni Yuvenal Shirima (659) Didas Lyamuya (329) Prosper Tesha (177) na Delphine Kessy (29)
"Namtangaza Enock Koola kuongoza kwa kura jimbo la Vunjo na Matokeo haya ni ya awali bado michakato ya chama inaendelea," amesema amahanyu.
Hii ni mara ya pili Koola anaongoza katika kura za maoni na mwaka 2020 katika mchakato wa ndani wa chama hicho, Koola aliongoza kwa kupata kura 187 na kufuatiwa na Dk Charles Kimei aliyepata kura 178 lakini Dk Kimei alipitishwa kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo.
Muheza
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Muheza na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma almaarufu (MwanaFA) ameongoza kwenye kura za maoni kwa kupata kura 9,030.
Akitangaza matokeo baada ya kupigwa kwa kura za maoni ndani ya CCM kusaka mpeperusha bendera yao katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 Msimamizi wa Uchaguzi katika Wilaya ya Muheza, Mwantumu Mahiza amesema kura zilizopigwa ni 10,320, kati ya hizo kura 60 zimeharibika.
Amesema jumla ya wagombea walikuwa sita amba oni pamoja na Hamis Ayubu aliyepata kura 339, James Edward kura 203, Hamis Sadiki kura 173, Togwe Msekelwa kura 122 na Halima Juma aliyeambulia kura 65.
Hai
Mbunge wa Jimbo la Hai aliyemaliza muda wake, Saashisha Mafuwe ameongeza kura za maoni zilizopigwa leo na wajumbe wa Chama cha Mapinduzi kumpata mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia chama hicho.
Mafuwe ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 4,973 kati ya 6,100 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo usiku huu, Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro, Elizabeth Minde amesema Mafuwe amepata kura 4,973 akifuatiwa na Fuya Kimbita aliyepata kura 557.
Wengine ni Jerry Muro aliyepata kura (274), Tumsifu Swai (106) na Apaisaria Kiwori aliyeambulia kura 47.
Mide amesema idadi ya wajumbe waliopiga kura ni 6,100, kura zilizoharibika ni 143 na kura hali ni 5,957.
Moshi vijijini
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Moris Makoi ameongoza kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Moshi vijijini, kwa kupata kura 2,148 na kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Profesa Patrick Ndakidemi aliyepata kura 627.
Akitangaza matokeo hayo leo, msimamizi wa uchaguzi, Ramadhani Mahanyu amesema kura zilizopigwa ni 4,649, zilizoharibika ni 60 huku halali zikiwa 4,589.
Mahanyu ambaye ni Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, amesema katika jimbo hilo wagombea walikuwa saba na aliyeshika namba tatu ni Felista Njau aliyepata kura 587, Salim Kikeke kura 491, Victor Tesha kura 409 huku Deogratius Mushi akipata kura 225 na Wilhad Kitaly akiambulia kura102.
Kigoma Mjini
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Kirumbe Ng’enda ameongoza kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuwashinda washindani wake katika kata zote 19 za jimbo hilo.
Katika mchakato huo wa kura za maoni uliowahusisha wagombea sita walioteuliwa, Kirumbe Ng’enda amepata kura 2,168 akifuatiwa kwa karibu na Clayton Revocatus maarufu Baba Levo, aliyepata kura 2,080.
Matokeo hayo yametangazwa usiku huuna Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Sadick Kadulo.
"Hayo ndiyo matokeo ya chama chetu kupitia kura za maoni. Hata hivyo, bado tunaendelea na mchakato kwa mujibu wa maelekezo na kanuni za uchaguzi, ikimpendeza Mungu tunaelekea hatua ya uteuzi rasmi," amesema Kadulo.
Amewatangaza wagombea wengine waliokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho kuwa ni pamoja na Dk Ahmad Sovu aliyepata kura 247; Baruan Muhuza kura 264; Dk Maulid Kikondo kura 180 na Moses Basila aliyepata kura 12.
Uyole, Mbeya Mjini
Wakati aliyekuwa Mbunge wa Mbeya mjini, Dk Tulia Ackson akishinda katika kura za maoni Jimbo jipya la Uyole, Patrick Mwalunenge naye amefanya kweli kwa kushinda Jimbo la Mbeya Mjini.
Uchaguzi huo ambao umefanyika leo umehusisha majimbo mawili ya Mbeya mjini na Uyole yenye jumla ya Kata 36 ukiambatana na kura za madiwani na kuhitimishwa saa 4:45 usiku kwa wasimamizi kutangaza matokeo ya jumla.
Akitangaza matokeo hayo usiku huu, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini, Mohammed Mavallah amesema Jimbo la Uyole lilikuwa na wapiga kura 5 148, ambapo Dk Tulia amepata kura 4,830.
Amesema katika Jimbo hilo, watiania walikuwa watatu wakiwa ni Dk Tulia aliyeongoza akifuatiwa Dk Seria Masole aliyepata kura 275 na Emir Sanga aliyepata 35.
Kwa upande wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mwalunenge ameongoza kwa kura 3,360 kati ya kura 5,211 zilizopigwa, ambapo watiania walikuwa sita.
Amesema Dk Mabula Mahande amepata kura 1,133, Shambwee Shitambala kura 392, Charles Makipesile (133), Sofia Malingumu (100) na Elizabeth Thobias kura 56.
"Kwa mujibu wa kanuni za CCM, hizi ni kura za maoni, hakuna mshindi hii ni kukirahisishia chama kupitia vikao vyake vya maamuzi, hivyo tunaomba utulivu na uvumilivu kwa kuwa tunaenda kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba,"amesema Mavallah.
Tanga
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu ameongoza kwenye kura za maoni katika uchaguzi uliofanyika jimboni humo kwa kupata kura 5,750.
Wengine walioshiriki kwenye uchaguzi huo ni Omar Ayoub (4,146), Rajabu Abas(130),Kassim Baraka (80) na Arif Fazel (70) ambapo wote kwa ujumla wao wamepigiwa kurs 10,293.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Chama cha Mapinduzi,(CCM) Wilaya ya Tanga, Jamal Abas amesema idadi ya wajumbe waliopiga kura kwa Tanga ilikuwa 12,620 ambapo kura zilizopigwa ni 10,293,zilizoharibika 117 na kura halali ni 10,176.
Amesema mshindi wa pili kwenye upigaji kura huo ni Omar Ayoub ambae kwa upande wale amepata kura 4,146 sawa na asilimia 40 ya kura zote ambazo zimepigwa na wajumbe hao.
Lindi Mjini
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Lawa amemtangaza Mohamed Utali kuwa mshindi wa kura za maoni kuwania ubunge katika Jimbo la Linid Mjini.
Katika uchaguzi huo uliofanyika, Lawa amemtangaza Utali kwa kupata kura 1,472 kati ya 3289 zilizopigwa huku mbunge anayemaliza muda wake, Hamida Abdalla akipata kura 876. Wagombea wengine Daud Msungu amepata kura 787, Yusuph Mwidadi 144 na Badru Mussa akimaliza na kura 17.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa matokeo zaidi