Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lilianza kuitwa Kombe la Mataifa huru ya Afrika

Muktasari:

Mashindano haya yalifanyika kwa mara ya kwanza, 1957. Tangu mwaka wa 1968, shindano hili hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Fainali za Afrika ni mashindano ya soka yanayojumuisha mataifa ya Afrika na kusimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Mashindano haya yalifanyika kwa mara ya kwanza, 1957. Tangu mwaka wa 1968, shindano hili hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Mwaka 1957 mataifa ya Misri, Sudan na Ethiopia yalishiriki kwa mara ya kwanza. Afrika ya Kusini ilikuwa ikishiriki, lakini ilizuiwa kutokana na sera za ubaguzi nchini humo. Kila mara yaliboreshwa na hadi sasa, Idadi ya wanaoshiriki fainali hizo wamefikia 16 tangu mwaka 1998.

Misri ndilo taifa lililofanikiwa zaidi katika historia kombe hili kwa kuwa na rekodi ya kushinda mara sita.

Ghana na Cameroon zimetwaa mara nne. Ghana na Cameroon zimeshinda matoleo mawili ya kwanza baada ya kila timu kushinda shindano hili mara tatu mfululizo.

Mashindano ya 1950-60

Chimbuko la Kombe la Mataifa ya Afrika lilikuwa Juni 1956, wakati uundaji wa CAF.

Mkutano wa Lisbon, Ureno ikiwa ni mkutano wa tatu wa Bunge la FIFA, kulikuwa na mipango ya haraka kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kufanyika na Februari mwaka 1957, shindano la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika lilifanyika mjini Khartoum, Sudan.

Hakukuwa na mechi za kufuzu katika shindano hili, kwani uwanja ulikuwa na mataifa manne ambao ndiyo wanzilishi wa CAF (Sudan, Misri, Ethiopia na Afrika ya Kusini). Kukataa kwa Afrika Kusini kupeleka kikosi chenye wachezaji wa rangi tofauti katika ushindani, kulisababisha kuadhibiwa na Ethiopia ilifuzu fainali.

Kutokana na tukio hilo, mechi mbili ndizo zilizochezwa na Misri kuwa bingwa wa kwanza Afrika baada ya kuishinda Sudan katika nusu fainali na Ethiopia katika fainali. Miaka miwili baadaye, Misri ndiyo ilikuwa mwenyeji wa pili wa fainali mjini Cairo na timu zile tatu ndizo zilizoshiriki. Misri ilitetea ubingwa kwa kuilaza Sudan katika fainali.

Timu ziliongezeka hadi kufikia tisa na ndizo zilizoshiriki shindano la mwaka 1962 mjini Addis Ababa na kwa mara ya kwanza kulikuwa na mechi za kufuzu na timu nne zilifuzu kuwania ubingwa.

Ethiopia kama mwenyeji, Misri bingwa mtetezi zilifuzu moja kwa moja na baadaye ziliingia Nigeria na Tunisia katika timu nne za mwisho zilizowania ubingwa. Misri ilicheza fainali kwa mara ya tatu, lakini Ethiopia walishinda baada ya kuipiga Tunisia katika nusu fainali kwa kuilaza Misri katika muda wa ziada.

Ghana yatawala

Mwaka 1963, Ghana ilishiriki kwa mara ya kwanza na kunyakua ubingwa kwa kuilaza Sudan katika fainali na kutwaa tena ubingwa miaka miwili baadaye.

Mfumo wa mashindano ulibadilika kwani 1968 ziliongezeka timu nane kuwania kufuzu kati ya timu 22 zilizofaulu awali. Timu zilizofaulu ziligawanywa katika makundi mawili, kila kundi likiwa na timu nne zilizocheza mechi za mzunguko na timu mbili bora ziliingia nusu fainali.

Mwaka 1992, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilitwaa ubingwa kwa kuilaza Ghana. Kuanzia mwaka 1968 fainali za Afrika zimekuwa zikifanyika baada ya miaka miwili na tangu wakati huo, mshambuliaji wa Ivory Coast, Laurent Pokou aliongoza kwa mabao katika michuano ya 1968 na 1970 kwa mabao sita mwaka wa 1968 na mabao nane katika mwaka wa 1970 na kushikilia rekodi kwa muda hadi 2008.

1970: Muongo wa mabingwa

Kati ya mwaka 1970-1980 mataifa sita yalitwaa ubingwa: Sudan, Kongo-Brazzaville, Zaire, Morocco, Ghana, na Nigeria. Zaire (DR Congo) ilishinda mara ya pili katika mwaka wa 1974 (ilishinda mara ya kwanza kama DRC) baada ya kupambana na Zambia katika fainali.

Morocco ilitwaa ubingwa mwaka 1976 nchini Ethiopia na Ghana ilitwaa mara ya tatu mwaka wa 1978. Mwaka wa 1980 fainali zilifanyika Nigeria na wenyeji Nigeria kuilaza Algeria na kunyakuwa ushindi mara ya kwanza. Mwaka huu Tanzania ilicheza kwa mara ya kwanza na mwisho.

1980: Kutawala kwa Cameroon na Nigeria

Ghana ilitwaa ubingwa mara ya nne mwaka wa 1982 baada ya kuishinda Libya kama mwenyeji katika fainali. Hii mechi iliisha sare ya bao 1-1 baada ya dakika 120 na Ghana ilishinda katika penalti na kunyakua taji.

Cameroon ilitwaa ubingwa mwaka wa 1986 kwa kuifunga Misri na 1988 ilitetea taji kwa kuifunga Nigeria mwaka wa 1984. Mwaka wa 1990, bingwa alikuwa Algeria.

Washiriki waongezeka mwaka 1992

Mwaka 1992 Fainali za Afrika zilipanuka, idadi ya washiriki ilifikia 12. Timu ziligawanywa katika makundi manne yenye timu tatu na timu mbili za juu ziliingia robo fainali. Mwaka huo, Ivory Coast ilitwaa ubingwa.

Miaka miwili baadaye, Nigeria, ilitwaa ubingwa kwa kuishinda Zambia, ambayo mwaka mmoja kabla ilipatwa na msiba wa wachezaji wake kuanguka katika ajali ya ndege kwenye mwambao wa Gabon.

Afrika ya Kusini ilikuwa mwenyeji mwaka wa 1996 na ilishiriki mara ya kwanza baada ya kupewa fursa ya kushiriki katika shindano hili walipoacha ubaguzi.

Idadi ya washiriki katika fainali iliongezeka hadi timu 16 ambazo ziligawanywa katika makundi manne. Hata hivyo, idadi halisi ya timu zilizocheza katika fainali mara ilikuwa 15 tu kwani Nigeria ilijiondoa katika dakika ya mwisho kwa sababu za siasa katika nchi yao.

Timu ya Bafana Bafana ilishinda taji kwa mara ya kwanza kwa kuilaza Tunisia wakati mwaka 2000 ubingwa ulikwenda kwa Cameroon baada ya kuishinda Nigeria katika penalti. Mwaka wa 2002, The Indomitable Lions ilipokea taji mara ya pili mfululizo kama Ghana ilivyofanya katika miaka ya 1960 baada ya Misri kufanya vivyo hivyo mwaka 1957 na 1959.

Mwaka 2006 fainali zilifanyika Misri ndipo iliweka rekodi ya kuwa washindi mara tano. Shindano la 2008 lilifanyika Ghana na Misri ikatetea ubingwa mara sita kwa kuilaza Cameroon 1-0 katika fainali. Misri iliweka rekodi Fainali za 2010 zilizofanyika Angola kwa kutwaa ubingwa mara ya tatu kwa kuilaza Ghana 1–0 katika fainali.

Mei 2010, ilitangazwa kuwa fainali zitachezwa miaka ya namba witiri ili isiingiliane na Kombe la Dunia. Zikachezwa Fainali 2012 zilizoandaliwa na Gabon na Guinea ya Ikweta na mwaka 2013 Afrika Kusini ikawa mwenyeji.

Mwaka 2012, Zambia ilitwaa ubingwa kwa kuilaza Côte d’Ivoire kwa mikwaju ya penalti. Hii ilionyesha kuwa mizimu ya wachezaji wa Zambia walioanguka kwenye mwambao wa Gabon, 1993 waliisimamia timu yao.

Nigeria ilitwaa ubingwa mwaka 2013 kwa kuilaza Burkina Faso wakati mwaka 2015 mashindano yalipangwa kufanyika Morocco, lakini waligoma wakihofia ebola, Guinea ya Ikweta ikaandaa na Ivory Coast ikatawazwa mabingwa.