Erick; nataka kuwa kama Usain Bolt

Muktasari:
Balozi Pastor Ngaiza ni moja kati ya wazazi wachache nchini wanaostahili kupewa pongezi kwa kile nilichokiona mimi kuwa anajali kile wanachokifanya watoto wake.
Balozi Pastor Ngaiza ni moja kati ya wazazi wachache nchini wanaostahili kupewa pongezi kwa kile nilichokiona mimi kuwa anajali kile wanachokifanya watoto wake.
Nilimkuta Mzee huyu katika majengo ya ofisi za Chama cha Riadha Tanzania (RT) zamani zikitumika kama ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) akiwa ameacha shughuli zake binafsi na kwenda kumtambulisha mtoto wake wa mwisho Erick Ngaiza ambaye ni mwanariadha wa mbio fupi za mita 100, 200, 400 pamoja na (400 relay) mbio za kupokezana vijiti.
Erick ambaye kwa sasa ameelekea nchini Afrika Kusini kusoma katika chuo kikuu cha Pretoria, anaamini katika miaka mitano ijayo anatarajia kufanya miujiza zaidi katika mchezo wa riadha baada ya kuchuja michezo yote ambayo awali alikuwa akiicheza.
Balozi Ngaiza anasema niligundua jambo kutoka kwa mwanangu kwa kuwa ilikuwa haipiti muda Erick alipasua vioo vya madirisha kwa kuvipiga na mpira na siku zilivyozidi kwenda niligundua ana kipaji cha kucheza mpira, lakini siku zilivyozidi kwenda niligundua ana kipaji kingine katika mchezo wa riadha.
Mbali na mchezo wa soka na riadha, Erick pia alibahatika kucheza michezo mbalimbali ambayo alishindwa kuendelea kuicheza kutokana na mazingira aliyokuwa nayo hasa katika upande wa masomo.
Michezo hiyo mingine ambayo anaweza kuicheza kwa kiwango cha juu ni pamoja na kuruka chini ( long jump), kuruka juu (high jump), kriketi, mpira wa wavu, Rugby, mpira wa meza, karate na kuogelea urefu wa mita 50.
Alibahatika kupata elimu ya msingi katika shule ya St Marys Mbagala na baada ya hapo alijiunga na shule ya sekondari Sisekelo iliyopo Botswana kidato cha kwanza mpaka cha sita na sasa amekwenda nchini Afrika ya Kusini katika chuo kikuu cha Pretoria kwa ajili ya masomo ya ufundi wa ndege.
Erick anasema michezo yote anaamini anaweza akaisahau, lakini siyo mchezo wa riadha kwani ndoto zake ni kuja kuwa kama mwanariadha maarufu duniani Mjamaica Usain Bolt.