Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simu za mkononi sasa ni zaidi ya mawasiliano

Baadhi ya simu kama hizi zina programu inayoweza kupima mapigo ya moyo. Picha zote na mtandao

Muktasari:

Kwa nchi zilizoendelea, simu zinatumika kama zana mojawapo ya ulinzi wa nyumba na katika tiba.

 

 

Uzoefu unaonyesha teknolojia ya simu za mkononi bado haijawawezesha Watanzania wengi kuzitumia katika masuala ya kimaendeleo hasa katika kurahisisha maisha.

Ukiondoa mawasiliano, Watanzania wengi wamezigeuza simu kama vyombo vya kuwaburudisha kama ilivyo kwa Athanas Sule (jina siyo lake).

Siku, wiki mwezi vyote vimepita hajafanya chochote katika simu yake zaidi ya kuitumia kwa salamu, kufanya utani na kupiga soga na rafiki zake katika mitandao ya kijamii hasa facebook.

Kipindi chote hicho hakuwahi kutumia simu kwa shughuli za maendeleo kama vile kuzungumza na mwalimu  wa mtoto wake, kujua bei ya masoko ya bidhaa, kujua hali ya hewa au hata kuomba ushauri kwa daktari.

Sule anawawakilisha Watanzania wengi ambao  wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama),  wanasema wamekuwa mstari wa mbele kutumia simu kwa masuala  ya burudani badala ya  kuzitumia kama zana muhimu ya maendeleo kama ilivyo katika nchi zilizoendelea.

 

Takwimu za simu

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA)  Profesa John Nkoma, Tanzania ina laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656.

Kwa idadi hiyo, Tanzania inatajwa kushika nafasi ya tisa kwa nchi za Kusini mwa bara la Afrika, huku ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki.

Mwaka 2014, ripoti ya masuala ya mawasiliano iitwayo Sub Saharan Africa Ericsson Mobility, ilionyesha kuwa asilimia 25 ya watu wanaotumia simu za kisasa wanapata huduma zao za malazi, chakula, elimu na habari kupitia mitandao ya intaneti iliyomo katika simu.

 

Matumizi ya simu

Mdau wa Tehama, Stansalaus Komba anasema, kwa wengi bado simu ni chombo cha burudani, kujionyesha na kujikweza.

“Wapo wanaonunua simu siyo kwa sababu ya kusukumwa na programu zake, bali uzuri wa kifaa husika hasa mwonekano wake, jina la simu. Haya yote ni kwa sababu wanalenga kutumia simu kwa minajili ya kuwaonyesha wengine,’’ anaeleza na kuongeza:

“Vilevile uko uthibitisho kuwa simu zinatumika kurubuni; hata wanaume wakware wanatumia simu kama chombo cha kuwanasa wanawake wenye tamaa.

Kwa upande mwingine, wapo Watanzania waliofunguka macho, wanazitumia simu kwa mtazamo wa maendeleo akiwamo mfanyabiashara wa chakula, Michael Baba anayeisifu teknolojia ya simu ya mkononi kwa kumrahisishia mawasiliano na wateja wake.

“Nafanya kazi kwa simu, wasichana hupeleka chakula badala ya kwenda kuuliza oda, siku simu ikiwa haina chaji napata tabu, siwezi kufanya hii kazi bila simu,” anaeleza.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, Godwin Gondwe, anasema simu ni kifaa muhimu kwa maisha ya binadamu, kwa kuwa kinaokoa muda na fedha, huku ikiondoa mipaka ya upashanaji habari kwa watu walio maeneo tofauti.

“Tunaishi kwenye dunia ya mawasiliano ambayo haishikiki wala kuonekana lakini ipo. Hivi sasa hakuna umbali wala ugeni, kila kitu kipo kwenye simu,’’ anasema.

 

Matumizi tofauti ya simu katika nchi zilizoendelea

Matumizi ya simu ya simu katika nchi zilizoendelea yamekwenda mbali; unaweza kusema ni muujiza lakini ndivyo ilivyo. Katika nchi hizo na hata baadhi ya watu wenye fedha katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, simu zinatumika katika tiba, zinafungua milango na mageti, zinatumika kama kinga kwa wahalifu.

Hii ni kutokana na programu mbalimbali ambazo watumiaji huzipakua na kuziingiza katika simu, tuone baadhi ya programu hizo:

Programu ya August

Kampuni ya Apple bado inaendelea kuifanya simu yako kuwa bora kwa matumizi tofauti na imeleta kitu kipya kiitwacho August, hiki unakipakua kwenye simu aina ya iPhone, iPod, au iPod touch na kukitumia kama ulinzi kwa kuangalia nani anaingia, nani anatoka ndani ya nyumba yako hata kama haupo.

Huhitaji kuwa na namba za siri, bali unabonyeza kitu kiitwacho iOS na kuchagua au kuuliza nani anaingia na kutoka, baada ya kukuonyesha ishara kuwa kuna mtu anayekaribia kwenye mlango wa nyumba yako. Aidha, kifaa hiki hukuwezesha kufunga na kufungua mlango kokote uliko.

 

Gogo gate

Kifaa hiki ni maalumu kwa ajili ya kufungua mageti na milango ya gereji, ukishapakua kwenye simu yako kinafanya kazi kwa kuwezeshwa na programu ya Wi-fi ya kwenye simu. Kina uwezo wa kufanya kazi kwa zaidi ya milango mitatu kupitia simu, tabiti na kompyuta.

 

Loxon

Kifaa hiki ukikipakua kitakuwezesha kufunga na kufungua mapazia ya nyumbani ukiwa ndani au nje ya nyumba na kwa umbali uliotegesha.

Kwa simu za Adroid za kisasa ikiwamo zile za Apple, mhusika hukipakua na kukielekeza kazi ya kufanya.

Kifaa hiki pia huweza kufanya kazi kwa mazoea, iwapo kitategeshwa, muda maalumu wa kufunga au kufungua mapazia ya nyumbani hufanya hivyo wakati ukifika bila kubonyezwa, bali huonyesha ishara kuwa tayari kimefanya kazi huku kikipewa msaada mkubwa na mtandao wa simu husika.

Kifaa hiki pia kinaweza kutumika kuwasha muziki na kuzima ukiwa mbali na nyumbani au ndani. Pia, unaweza kuzima, kuwasha taa, kutegesha mlio wa tahadhari ya hatari.

 

HealthMyVitals

Licha ya wataalamu wa afya kupinga simu kutumika kupima mapigo ya moyo, lakini watu katika nchi zilizoendelea hupakua kwenye simu kifaa kiitwacho Pros, Cons na kuunganisha kwenye faili liitwalo iHealthMyVitals na kuwezeshwa kupima mapigo ya moyo.

 

Netra

Hii ni programu unayoweza kuweka kwenye simu na ikakueleza kama una tatizo la macho na unahitaji miwani ya aina fulani.

Siyo kuelewa kuwa una tatizo la macho, bali pia kinafafanua ni tatizo gani, ufanye nini ili lisiendelee, au unatakiwa kuvaa miwani aina gani.

Mtaalamu wa kifaa hicho Profesa Manuel Oliveira anasema kuwa kwa sasa kinafanya kazi katika nchi zilizoendelea, lakini baadaye watahakikisha kinafika hadi kwenye nchi zinazoendelea.