Mapishi: Biskuti za kahawa

Muktasari:
- Pamoja na kuwepo kwa aina nyingi ya biskuti, kumekuwepo na tofauti ya ladha. Hii hutokana na kutofautina kwa viungo kati ya biskuti moja na nyingine.
Pamoja na kuwepo kwa aina nyingi ya biskuti, kumekuwepo na tofauti ya ladha. Hii hutokana na kutofautina kwa viungo kati ya biskuti moja na nyingine.
Hilo ndilo jambo linalozifanya biskuti za kahawa kuwa tofauti na biskuti za aina nyingine.
Mahitaji
Unga wa keki kilo moja
Chumvi nusu kijiko cha chai
Sukari nusu kilo
Siagi robo kilo
Mafuta ya kupikia kiasi
Baking powder kijiko kimoja cha chakula
Vanilla matone matatu
Kahawa vijiko viwili
Vya kujazia
Maji robu tatu kikombe cha chai
‘Icing sugar’ 200g
Siagi gramu 100
Maziwa robo tatu kikombe cha chai
Namna ya kutengeneza
Kwenye bakuli moja kubwa, weka unga wa ngano, chumvi, baking powder na sukari. Changanya vizuri, kisha chukua siagi na anza kukanda.
Weka matone matatu hadi manne ya vanilla. Chukua maji kidogo na weka kwenye mchanganyiko wako, huku ukiendelea kukanda hadi liwe donge gumu.
Funika na uache ukae kwa muda wa saa 12. Ikiwa umekanda usiku unaweza kuuacha hadi asubuhi.
Sukuma kama chapati, kisha kata katika umbo la biskuti. Kata na zipange kwenye bati la kuokea. Oka kwa muda wa dakika 8-12 kwa moto wa kawaida.
Vya kujazia: Chukua donge la kahawa na weka kwenye maji, koroga na kisha weka kwenye sufuria. Weka viungo vingine kama maziwa, siagi na sukari. Injika jikoni acha vichemke. Koroga kwa muda wa dakika tano kwa kutumia mwiko. Ipua na acha vipoe.
Baada ya hapo chota kidogo na tandaza kwenye uso wa biskuti moja na kisha weka nyingine juu yake. Fanya hivyo kwa biskuti zote.
Biskuti zako zipo tayari kwa kuliwa. Unashauriwa kuhifadhi katika chombo chenye mfuniko.
Email:[email protected]