WWF waikabidhi serikali ndege zisizo na rubani kudhibiti ujangili
Muktasari:
Ndege hizo zitawekwa katika mbuga na hifadhi ili kuchukua picha katika maeneo mbalimbali na kurudisha majibu.
Dar es Salaam. Shirika la Wanyamapori Duniani (WWF) limeikabidhi serikali ndege nane zisizo na rubani (drones) zenye thamani ya Sh 60 milioni kwa ajili ya kupambana na ujangili.
Ndege hizo zitawekwa katika mbuga na hifadhi ili kuchukua picha katika maeneo mbalimbali na kurudisha majibu.
Mwakilishi Mkurugenzi WWF nchini Meneja Uhifadhi Simon Lugangu amesema ndege hizo zisizo na rubani zitachukua picha, kisha kuzihifadhi katika kompyuta na zitawasaidia askari wa maliasili kupata taarifa za majangili.
Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Majangili Kanda ya Kusini, Joshua Mmari alizungumzia kupungua kwa tembo nchini na kusema katika kipindi cha miaka ya 1970 kulikuwa na tembo 110,000 lakini hadi 2014 idadi yao ilipungua na kubaki 15,000.