Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

William Lukuvi afariki dunia kwa mshituko wa moyo

Aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi enzi za uhai wake.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi (70) amefariki dunia saa 1:00 asubuhi ya leo Jumatano, Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kifo hicho kimetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka juu ya msiba huo wa Lukuvi aliyezaliwa Agosti 15, 1955.

Taarifa hiyo imeeleza Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isiman, Mkoa wa Iringa amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

“Rais anatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo,” amesema Dk Kusiluka.

Lukuvi alikuwa miongoni mwa wabunge waandamizi bungeni ambaye amekuwa mbunge wa Ismani kuanzia mwaka 1995 hadi sasa akihudumu kwa zaidi ya miaka 30.