Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wavuvi watoa ya moyoni wakiililia Serikali Zanzibar

Muktasari:

  • Hayo yalisemwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi za Maji na Uvuvi,Dk Benaisha Benno alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa Habari juu ya uharibifu wa mazingira kwenye bahari.

Utafiti wa mwaka 2014 unaonyesha asilimia 90 ya wavuvi nchini wanatumia zana duni hali inayosababisha kuvua samaki tani 52,000 kwa mwaka ambao ni tofauti na rasilimali zilizopo kwenye bahari ya Hindi.

Hayo yalisemwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi za Maji na Uvuvi,Dk Benaisha Benno alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa Habari juu ya uharibifu wa mazingira kwenye bahari.

Benno alisema wavuvi hao hawana vifaa vya kisasa vitakavyowasaidia kuvua samaki katika bahari kuu matokeo yake wanashindwa kuvua samaki wakubwa na wengi ili waweze kujipatia kipato cha kuendeshea maisha yao.

Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri),Baraka Kuguru alisema sekta ya uvuvi ikipewa kipaumbele itachangia ukuaji wa uchumi na hivyo kutekeleza malengo ya viwanda na u humi wa kati.

Kuguru alisema tafiti zinaonyesha kwamba sekta ya uvuvi imekuwa na mchango mkubwa kwa nchi ambazo zimewekeza hasa katika ukanda wa bahari ambapo rasilimali zilizopo kwenye bahari zina thamani ya dola za Marekani 333 bilioni huku uwekezaji ukiwa asilimia 20 mpaka sasa.

“Kinachotokea wavuvi wanatumia zana duni ikiwemo ngarawa,mitumbwi ambayo haiwezi kwenda bahari kuu kuvua samaki wengi na wakubwa matokeo yake wanapata wachache na kuvua tani 52,000 kwa mwaka tofauti na nchi ya Mauritius wanavua samaki tani 300 kwa mwaka,”alisema Dk Benno.

Mmoja wa wavuvi wa soko kuu la samaki la Zanzibar,Hamisi Arafat Hamisi aliiomba serikali iwatengenezee mazingira bora yatakayowawezesha kupata mikopo ili kuweze vitakavyowawezesha kununulia vifaa vya kisasa vitavyoweza kufika bahari kuu ambapo wataweza kuvua samaki aina ya jodari na papa.

Kwa upande wake Mvuvi Omary Hamis alisema changamoto iliyopo ukosefu wa boti yenye uwezo wa kuvuz katika kina kirefu hali inayosababisha kuvua samaki wadogo na wachache.

“Boti tuazotumia zinaweza kuvua mita isiyozidi 30 hivyo kupelekea kupata samaki wachache na wadogo,tunaiomba Serikali isifikilie kuchukua kodi ijikite kwenye uwekezaji wa sekta ya uvuvi kwani ina faida kwa nchi na wananchi,alisema Hamisi.