Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania 35 'waliozamia' Afrika Kusini watozwa faini Sh50,000

Washtakiwa 35 ambao ni Watanzania 'waliozamia' Afrika Kusini, wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kusomewa shtaka la kuondoka nchini kinyume cha sheria. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Wanakabiliwa na shtaka moja la kuondoka nchini Tanzania kwenda Afrika Kusini bila kuwa na kibali, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya mwaka 2000 hadi Juni , 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere( JNIA) uliopo Wilaya ya Ilala.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu Watanzania 35 kulipa faini ya Sh50,000, kila mmoja au kwenda jela miezi 12, baada ya kukiri shtaka la kuondoka ndani ya Tanzania na kwenda Afrika Kusini bila kufuata taratibu za Uhamiaji.

Waliohukumiwa adhabu hiyo katika kesi ya jinai namba 12285 ya mwaka 2026 ni Abdul Singa, Abdallah Mkelewale, Salim Salim, Nassoro Wage, Rahim Msabaha, Rajabu Salum, Hemedy Mputo, Salum Mitima, Kulwa Amkachi, Anold Temu na wengine 25.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamepelekwa mahabusu wakisubiri kulipa faini.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Juni 4, 2026 na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, baada ya washtakiwa kukiri kosa lao na Mahakama kuwatia hatiani kwa kosa hilo.

Hakimu Lyamuya alisema washtakiwa wametiwa hatiani kama walivyoshtakiwa na wamekiri wenyewe shtaka lao.

"Nimezingatia washtakiwa ni wakosaji wa mara ya kwanza na washtakiwa wote mmeomba msamaha mbele ya mahakama hii, hivyo nina wahukumu kila mmoja kulipa faini ya Sh50,000 na mkishindwa mtatumikia kifungo cha miezi sita 12 jela," amesema Hakimu Lyamuya 

Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu, Wakili wa Ezekiel Kibona akishirikiana na Mohamed Mlumba, walidai hawana kumbukumbu za makosa ya nyuma, hivyo waliomba Mahakama itoe adhabu kwa mujibu wa sheria.

"Mheshimiwa hakimu, upande wa mashtaka hauna kumbukumbu ya makosa ya nyuma ya washtakiwa hao, ila tunaomba mahakama iwape adhabu kwa mujibu wa sharia ili iwe fundisho kwa vijana wengine wanaokwenda nje ya nchi bila utaratibu," alisema Wakili Kibona.

Kwa upande wao washtakiwa, waliomba mahakama iwapunguzie adhabu kwani ni kosa lao la kwanza na hawatarudia tena na kwamba walitenda huko kwa sababu ya ugumu wa maisha.

Hakimu Aaron baada ya kusikiliza shufaa za washtakiwa hao aliwahukumu kila mmoja kulipa faini ya Sh50,000 na wakishindwa wanatakiwa kutumikia kifungo cha miezi 12 jela.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wamesomewa mashtaka yao na wakili Kibona, ambapo alidai

wanakabiliwa kosa moja ambalo ni kuondoka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na Kanuni ya 20(3)(a) na 37 cha kanuni za a za Uhamiaji, tangazo la Uhamiaji namba 657 la mwaka 1997.

Alidai washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Mei 29, 2026 katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA ) uliopo Wilaya ya Ilala, ambapo washtakiwa wakiwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waliondoka nchini Tanzania bila kufuata utaratibu wa sheria za uhamiaji na kwenda Afrika Kusini kwa wakati tofautitofauti.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa walikutwa wametoka isivyo halali katika ardhi ya Tanzania bila kibali na kueleleka nchini Afrika Kusini.