Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano wafariki ajalini Dodoma

Muktasari:

  • Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi la Arusha Express kugongana uso kwa uso na lori.

Dodoma. Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi la Arusha Express kugongana uso kwa uso na lori.


Ajali hiyo imetokea leo Jumapili Novemba 13, 2022 mchana eneo la Veyula Kata ya Makutupora mkoani Dodoma.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibiti ajali hiyo na kusema bado wanafuatilia chanzo cha ajali na athari zaidi zilizotokana na ajali hiyo.


"Ni kweli ajali hiyo ipo, watu watano wamepoteza maisha katika eneo la ajali na wengine kujeruhiwa na wamekinbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu," amesema Otieno.


Hata hivyo amesema taarifa kamili zitatolewa baadaye kwani Polisi walikuwa eneo la tukio kufuatilia.

Basi hilo lilikuwa linatoka Arusha kwenda Mbeya limegongana uso kwa uso na lori la kampuni ya ujenzi ya China Hydropower.



Taarifa zaidi kukujia…