Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wastaafu walia kupunjwa pensheni

Rais wa Umoja wa Wastaafu Tanzania (REAT)! Dauda Biligesi akisoma tamko lao

Muktasari:

  • Wastaafu nchini wameigongea mlango Serikali wakiomba kukaa nao mezani kujadili suala la mapunjo wanayo yapata kwenye malipo ya mfuko wa pensheni.

Dodoma. Baadhi ya wafanyakazi wastaafu nchini wameigongea mlango Serikali wakiomba kukaa nao mezani kujadili suala la mapunjo wanayo yapata kwenye malipo ya pensheni.

Kupitia viongozi wa Umoja wa Wastaafu Tanzania (REAT), wameandika barua wakiomba kukutana na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ili wazungumze changamoto zao ikiwemo suala la pensheni ambayo wanadai wanaibiwa.

Wastaafu hao wanasema wanadai kima cha chini cha pensheni cha Sh100, 125 ni kidogo kwa mujibu wa sheria na kudai kuwa hivi sasa walipaswa kulipwa Sh259, 000 na ndilo takwa la kisheria.

Akizungumza leo Januari 6 jijini hapa, Rais wa REAT Dauda Bilikesi amesema wameandika barua kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima ambaye wanamuomba kuwa balozi wao kwenye jambo hilo ili awakutanishe na Makamu wa Rais Dk Mpango wamueleze kilio chao.

Bilikesi amesema mapendekezo yao wanaomba Serikali na Bunge watambue kuwa wastaafu wote nchini kwa sasa wana umoja wao ambao umesajiliwa kisheria, hiyo watoe fursa ya kupokelewa kwa maoni yao na kusikilizwa kwani kuna changamoto nyingi kwao.

Amesema sheria inatamka kuwa mstaafu anapaswa kulipwa pensheni ya asilimia 40 ya kima cha chini cha mshahara 389,000 lakini takwa hilo halitekelezwi tangu walipopandisha mshahara 2015 chini ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Jakaya Kikwete.

“Hata sheria ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ikiwemo PSSSF inatambua hilo kwamba ni kinyume kulipa chini ya asilimia 40 ambazo zilipitishwa na Bunge, leo hii unapomlipa mtu kiwango ambacho kinampunja ni wizi,” amedai Bilikesi.

Kwa upande wake mjumbe wa REAT, Ezekiah Oluoch amesema kinachofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii ni wizi kwa madai hawafuati sheria inavyotaka hivyo wanaendelea kuwakandamiza wanyonge ambao kikokotoo kilishawaumiza kabla.

Oluoch ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) amesema kwa sheria ya sasa wakifuata kima cha chini cha mshahama ambacho ni Sh389,000, hivyo mstaafu wa kima cha chini alipaswa kulipa Sh155,610 lakini bado  cha Sh100,125 jambo alilosema linavunja sheria.

Juhudi za kutafuta upande wa serikali kufafanua madai hayo zinaendelea.