Wanachama AAAM watembelea kiwanda cha magari Tanzania

Muktasari:
- Wanachama wa umoja wa watengenezaji wa magari duniani (AAAM) wametembelea kiwanda cha magari cha GFA Kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Dar es Salaam. Wanachama wa umoja wa watengenezaji wa magari duniani (AAAM) wametembelea kiwanda cha magari cha GFA Kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Wakiwa nchini Tanzania wamekutana na viongozi wa Serikali na kuzungumza mambo kadhaa kuhakikisha lengo la Tanzania ya viwanda linatimia kwa vitendo.
Kiongozi wa msafara huo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Nissan ukanda wa Afrika ,Mike Whitfield amesema watashirikiana na kiwanda hicho cha GFA katika maeneo mbalimbali ili kiweze kujitegemea katika uunganishaji wa magari ili Tanzania kuwa kama nchi nyingine zinazotengeneza magari kama Afrika Kusini.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya GFA, Mehbooub Karmali ameshukuru ujio wa wanachama hao akibainisha kuwa wakiweza kufanya kila kitu katika kiwanda hicho itakuwa faida kwa Taifa.
Miongoni mwa wanachama wa umoja huo ni Nissan, Ford, BMW, Isuzu, Toyota na Volkswagen.