Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliorejea shuleni baada ya kujifungua waomba hosteli kuishi na watoto

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda

Muktasari:

  • Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB), Dk Victoria Kwakwa amesema wataendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili sekta hiyo ifanyiwe maboresho kuwezesha wanafunzi wengi kurudi masomoni.

Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatisha masomo kutokana na ujauzito wameomba kujengewa hosteli ambazo zitawasaidia kuishi na watoto wao.

Wamesema hosteli hizo zitawasaidia kuwa karibu na watoto wao kwa sababu kwa sasa wanakosa umakini wakiwa darasani kutokana na kuwa mabli nao.

Wametoa rai hiyo juzi wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB), Dk Victoria Kwakwa alipofanya ziara katika Shule ya Msingi Turiani ya kufuatilia utekelezaji wa mradi wa kuwarejesha masomoni wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na matatizo mbalimbali, ikiwamo ujauzito ambapo Shule hiyo ni mojawapo ya wanaotekeleza mradi huo.

Mmoja wa wanafunzi waliorejea masomoni baada ya kukatisha kwa miaka miwili kutokana na ujauzito, Joan Machange, alimuomba Dk Victoria waboreshewe miundombinu ya kujifunzia ili waondokane na mfumo wa kusoma nadharia.

“Tunaomba tujengewe hosteli kwa sababu tunatoka mbali, tunafika nyumbani tumechoka hivyo tunakosa muda wa kusoma, pia hii itatusaidia kuwa karibu na watoto wetu kwa sababu wakati mwingine tunakosa umakini darasani kutokana na mazingira tuliyowaacha watoto wetu,” alisema.

Kwa upande wake Dk Victoria amesema wataendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili sekta hiyo ifanyiwe maboresho kuwezesha wanafunzi wengi kurudi masomoni.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali ingewazuia wanafunzi hao kurudi masomoni kama wanatoka familia masikini ndoto zao zingeisha.

“Rais Samia aliagiza tuwarejeshe wanafunzi hawa wasome, tuna mkakati wa kuwarejesha watoto wote walioacha shule, tayari tumewarejesha watoto 3,333, kati ya hao 900 wamerejea kwenye mfumo wa elimu wa kawaida na wengine kupitia elimu mbadala na watachukua miaka miwili kumaliza elimu ya sekondari,” amebainisha Profesa Mkenda.