Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waganga wanavyodhalilisha wasichana kingono

Muktasari:

  • Bado jamii nyingi Tanzania na mtu mmoja mmoja wanaamini waganga wa kienyeji wana uwezo wa kutibu magonjwa mengi yaliyoshindikana hospitalini.

Bado jamii nyingi Tanzania na mtu mmoja mmoja wanaamini waganga wa kienyeji wana uwezo wa kutibu magonjwa mengi yaliyoshindikana hospitalini.

Hata hivyo, hukumu mbili za Mahakama ya Rufani za hivi karibuni dhidi ya waganga wawili wa kienyeji waliotiwa hatiani kwa kubaka na kudhalilisha wasichana kingono ni fundisho tosha kwa wazazi na walezi wanaowaamini kupitiliza.


Mganga abaka mtoto wa miaka sita

Moja ya kesi zinazofichua jinsi waganga wa kienyeji wanavyoweza kugeuka hatari kwa mtoto wa kikeni ile inayomhusu Barnaba Chagalo, ambaye hivi karibuni amepoteza rufaa ya kupinga kifungo cha miaka 30 kwa kumbaka msichana wa miaka sita mwaka 2014 katika Kijiji cha Milala, Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi.

Changalo alikuwa mganga maarufu. Oktoba 26, 2014 alitembelea nyumba ya mama mmoja (jina linahifadhiwa) ambaye aliishi na wajukuu zake wawili wa kike na wa kiume (majina yanahifadhiwa).

Alipokelewa na kulala katika nyumba hiyo, asubuhi ya siku iliyofuata mjukuu wa kiume wa mama yule alikwenda shamba huku wa kike akielekea shuleni.

Bibi yao alikuwa mgonjwa, hivyo alibaki nyumbani akifanya shughuli ndogondogo. Wakati huo, mganga yule aliendelea kumtibu kwa kumpatia dawa.

Baadaye mjukuu wa kike wa mama yule alirudi nyumbani akitokea shuleni. Kwa kuwa alikuwa na jeraha katika mkono wake, mganga huyo alianza kumtibu kwa kumsugua na dawa za kienyeji.

Baada ya kumtibu, Changalo aliingiwa tamaa mbaya. Alimchukua binti yule hadi chooni, akavua suruali yake na kisha kumvua nguo yule msichana na kuanza kumbaka.

“Nilihisi maumivu makali lakini sikuweza kupiga kelele kwa kuwa mrufani (mbakaji) aliniziba mdomo,” mwathirika huyo aliiambia Mahakama ya Wilaya ya Mpanda aliposhitakiwa mbakaji.

Wakati mganga huya akiendelea kumnajisi binti yule, bibi yake alikwenda chooni kwa ajili ya haja ndogo na kukuta mlango wa choo umefungwa. Alipogonga, Changalo alimjibu kuwa ni yeye ndiye aliyekuwa ndani.

Mama yule aliendelea kumsubiri Changalo amalize haja yake, lakini muda ulipita bila kutoka. Kuchelewa kwa Changalo kutoka chooni kulimpa wasiwasi yule mama ambaye aliamua kuchungulia kwa dirishani na kushuhudia mambo ya kutisha. Alimwona mganga yule akimbaka mjukuu wake.

Baadaye mganga yule alikamatwa na kushtakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda. Alitiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Katika utetezi wake, Changalo alidai kuwa kesi dhidi yake ilikuwa ya kubambikiwa na bibi wa mwathirika ili kukwepa kumlipa Sh200,000 alizodai kumdai kama gharama ya kumtibu mguu wake na matatizo mengine bibi aliyodai amelogwa.

Changalo alikata rufaa dhidi ya kutiwa hatiani na kifungo katika Mahakama Kuu, lakini rufaa yake ilitupiliwa mbali. Baadaye alikata rufaa ya pili Mahakama ya Rufaa akidai kesi dhidi yake haikuthibitishwa bila kuacha shaka.

Hivi karibuni majaji wa Mahakama ya Rufani, Shaban Lila, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo wameitupilia mbali rufaa yake, lakini wakapunguza kifungo cha maisha kuwa cha miaka 30, wakisema upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kuwa mwathirika alikuwa na umri chini ya miaka kumi.

Hadi Januari 21, 2017, msichana wa miaka 14, Ukae (si jina halisi) alikuwa akiishi na mama yake wa kambo eneo la Kibaoni, Wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.

Siku hiyo majira ya saa 12:30 jioni, Ukae alikuwa akicheza nje ya nyumba yao pale mganga wa kienyeji maarufu katika eneo hilo, Masanja Makunga alipopita karibu na nyumba yao na kumwomba msichana huyo amfuate nyumbani kwake.

Alimwambia anakwenda naye kumtengenezea kinga dhidi ya mashetani ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Akiamini kuwa Makunga alikuwa mtu mwema, Ukae alikubali kumfuata hadi kwenye chumba alichopanga jirani na kwao katika nyumba ya mwanamke mmoja.

Wakati Makunga akiwasili na binti yule, mwanamke huyo alikuwa nje ya nyumba yake akifanya shughuli za nyumbani, aliingia naye ndani ya chumba chake na kumwacha nje mdogo wake Ukae wa kiume ambaye aliwafuata kwa nyuma hadi nyumbani kwa mganga yule.

Ndani ya chumba chake, mganga huyo alitumia zaidi ya nusu saa na binti yule. Mdogo wake Ukae ambaye alikuwa nje ya chumba hakuweza kushuhudia kilichokuwa kinaendelea ndani, lakini ni Ukae mwenyewe ambaye alikuja kufichua yaliyompata ndani ya chumba cha mganga.

Aliiambia Mahakama ya Wilaya ya Kilosa ambapo Makunga alishtakiwa kwa udhalilishaji wa kingono kwamba wakiwa ndani ya chumba chake, Makunga alimtaka avue nguo zake na kuchuchumaa.

Kwa mujibu wa ushahidi wa Ukae, kilichofuata kilimtisha sana. Alidai kuwa mganga yule alichukua kiwembe na kuanza kuchanja sehemu mbali mbali za mwili wake na kumpaka dawa na pia alimnyoa sehemu za siri.

Mwathirika huyo alidai kwa wakati huo wote, mganga yule alikuwa amevua nguo zote na kubakiwa na nguo ya ndani tu.

“Mrufani (Makunga) aliniambia nipanue miguu yangu lakini nikakataa kwa sababu nilikuwa kwenye hedhi,” binti huyo aliiambia Mahakama.

Alipogundua kuwa haitakuwa rahisi kutekeleza nia yake ovu, Makunga aliamua kumkalisha binti yule katika mapaja yake na kuanza kumnyonya masikio na mdomo hadi alipomaliza haja yake. Baada ya muda alimwachia na kumsindikiza kwao huku akimtaka asieleze yaliyofanyika kwake.

Alipofika nyumbani, mama wa binti huyo tayari alikwishakuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa binti yake. Alipomuuliza alikuwa wapi, binti yule alimsimulia mama yake wa kambo ambaye aliripoti suala hilo kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa aliyefanikisha kukamatwa kwa Makunga.

Baada ya kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashahidi sita, Mahakama ya Wilaya ya Kilosa ilimtia hatiani Makunga na kumhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela.


Kosa la hakimu lamnusuru Makunga

Jaribio la kwanza la Makunga kutaka aachiwe huru lilishindwa mwaka 2018 baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali rufaa yake na kuithibitisha hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Kilosa. Hata hivyo, hivi karibuni Mahakama ya Rufani imemwachia huru baada ya kugundua makosa katika usikilizwaji wa kesi hiyo.

Mahakama ya Rufani imekubaliana na Makunga kuwa hakimu aliyesikiliza kesi dhidi yake katika Mahakama ya wilaya alimhoji mtoto aliyedaiwa kubakwa ili kujiridhisha kuwa mtoto huyo alikuwa anajua maana ya kiapo.

Kifungu cha 127 (2) cha Sheria ya Ushahidi kinamtaka hakimu kumwapisha mtoto wa umri wa chini ya miaka 14. Katika hatua hii, hakimu humuuliza maswali machache ili mtoto huyo aahidi kuiambia Mahakama ukweli tupu na si uongo kabla ya kuanza kutoa ushahidi.

Sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2016 na kuondoa hitaji la Mahakama kumhoji mtoto ili kujua uwezo wa kuwa shahidi.

“Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alitakiwa kufuata msimamo mpya wa sheria unaotaka mtoto wa umri wa chini ya miaka 14 kuhojiwa na kutoa ahadi ya kusema ukweli na si uongo kabla ushahidi wake kupokelewa mahakamani.

Hakuna maelezo katika rekodi kwamba takwa hilo la kisheria lilizingatiwa, mwathirika hakutoa ahadi hiyo,” walisema majaji Shaban Lila, Mwanaisha Kwariko na Ignus Kitusi katika uamuzi wao wa hivi karibuni.