Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachanga vifaa vya Sh110 milioni kuiwezesha hospitali

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini,Dk Tulia Ackson(wa pili kushoto) akipata maelezo ya namna ya matumizi ya mashine ya upasuaji kwa wakinamama wajawazito  inavyofanya kazi Mara baada ya kukabidhiwa  na  wadau na wananchi mkoani hapa. Picha na Hawa Mathias.

Muktasari:

  • Imeelezwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi kwa  wakinamama wajawazito  wakati wa kujifungua.

Mbeya. Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya imekabidhiwa vifaa vya kisasa, ikiwemo mashine ya upasuaji na kitanda maalumu cha kujifungulia kwa wajawazito.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh110 milioni vimetolewa kupitia michango ya wananchi na wadau mbalimbali kutoka Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja (UTT AMIS) tangu mwaka 2023.

Akizungumza leo Alhamisi Desemba 12, 2024, Mdau wa Maendeleo, Noela Msuya amesema lengo la kuchangia vifaa hivyo ni kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya kwa wanawake na wajawazito.

Msuya amesema fedha hizo zilitokana na harambee ya kuchangia huduma za afya iliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2020, Sh110 milioni.

Amesema mwaka 2023, fedha hizo ziliwekezwa kwenye Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja (UTT AMIS) na kufikia Sh126 milioni 126, ikijumuisha faida ya Sh16 milioni.

"Baada ya faida hiyo, tulijadili na kutenga shilingi milioni 110 kwa ajili ya kununua mashine ya upasuaji, kitanda cha kisasa na mifuko 448 ya saruji," amefafanua Msuya.

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson ambaye amepokea vifaa hivyo kwa niaba ya uongozi wa hospitali, amesema  msaada huo utasaidia kuboresha huduma za kitabibu kwa wajawazito.

Dk Tulia amesisitiza kuwa vifaa hivyo vitaongeza ufanisi katika huduma za afya licha ya changamoto ya uhaba wa vifaa.

"Vifaa hivi ni matokeo ya mchango wa wananchi na wadau wa Mkoa wa Mbeya waliotambua umuhimu wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, walijichanga kwa fedha taslimu na ahadi mbalimbali,” amesema Dk Tulia.

Aidha, amesema kabla ya ununuzi wa vifaa hivyo, wadau walipanga kujenga wodi ya wajawazito, lakini serikali tayari imefanya maboresho makubwa kwenye sekta ya afya ikiwamo ujenzi wa wodi mpya na kukarabati zilizochakaa.

Katika ziara hiyo, Dk Tulia pia amekagua visima vya maji katika Kituo cha Afya Iyela na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iduda, ambako kulikuwa na kero ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Rehema Jackson, mjamzito aliyefika hospitalini hapo kupata huduma, amesema uwepo wa vifaa hivyo utasaidia kupunguza vifo vya wajawazito.

“ukosefu wa vifaa na huduma jirani ni moja ya mambo ambayo yanachangia sana vifo vya wanawake wajwazito, tunashukuru kwa hiki kilichofanyika,” amesema Jackson.