Wabunge wataka mwekezaji arejeshe hoteli 3 zilizokufa

Muktasari:

  • Wabunge hao wametoa kero zao wakati wakichangia kwenye taarifa za Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii.

Dodoma. Mbunge wa Nsimbo, Taska Mbogo amependekeza Serikali kumnyang'anya mwekezaji aliyechukua hoteli kubwa tatu nchini, akisema hana uwezo na anakiuka mkataba.

Mbogo amezitaja hoteli hizo ni Embassy, Kunduchi Beach na Mikumi, akisema zilichukuliwa na mwekezaji mmoja lakini miaka 14 Sasa ameshidwa kufanya hata ukarabati.

Akichangia bungeni leo ubinafsishaji kwa baadhi ya maeneo haukuwa na tija hivyo ukipaswa kuangaliwa ikiwemo kwenye rasilimali za nchi.

"Tulikuwa na hoteli kubwa 23 lakini tulikwenda kwenye sera ya ubinafsishaji ambao baadhi ya maeneo imeshindwa kutusaidia, tunaomba zirudishwe Serikalini ili zitusaidie kwa watalii," amesema Mbogo.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Florence Samizi amesema mpango huo umeiumiza Serikali tena ni aibu kwa Serikali kwani baadhi ya hoteli ikiwemo Musoma zimegeuka kuwa vichaka.

Dk Samizi amesema hoteli sita hazijafanyiwa kazi na baadhi zimeshaombwa kurudishwa kwa Shirika la Reli Tanzania, kwani zimekufa tangu 1992.

Amesema kuna sheria inayotaka mtu akishindwa kuendeleleza ananyang'anywa lakini sheria haitamki waliobinafsishwa mahoteli kama wanaweza kutakuwa kumnyang'anywa.