Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vyandarua milioni 20 vyasambazwa Tanzania

Muktasari:

  • Vyandarua vilisambazwa kupitia Mradi wa Kudhibiti Vidudu vya Malaria wa Rais wa Taifa hilo (PMI) ambao umekamilika.

Dar es Salaam. Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (Usaid) limesema Mradi wa Kudhibiti Vidudu vya Malaria wa Rais wa Taifa hilo (PMI) umekamilika.

Kwa mujibu wa Usaid, katika mradi huo wa miaka minne zaidi ya vyandarua milioni 20 vilivyotiwa dawa vilisambazwa Tanzania Bara na Zanzibar na kulinda zaidi ya watu milioni 35.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Misheni ya Usaid, Craig Hart waliwezesha usambazaji huo wa vyandarua kupitia kampeni katika shule na vituo vya afya, ikilenga makundi hatarishi kama vile watoto wachanga na wajawazito.

"Ushirikiano wa Marekani na Tanzania unachukua zaidi ya miongo sita na tangu mwaka 2006, PMI imewekeza zaidi ya Dola milioni 747 kukabiliana na malaria nchini Tanzania.

"Tunajivunia mafanikio ya mradi wa PMI. Ingawa mradi huu mahususi umekamilika, dhamira yetu ya kushirikiana na watu wa Tanzania kukabiliana na ugonjwa wa malaria na changamoto nyingine za afya ya jamii bado haijayumba,” amesema.

Kuanzia mwaka 2020 hadi 2024, mradi wa Dola milioni 43, ukiongozwa na Kituo cha Johns Hopkins cha Mipango ya Mawasiliano kwa ushirikiano na Tropical Health LLP na Viamo PBC, uliunga mkono juhudi za kulinda asilimia 90 ya watu walio katika hatari.

Juhudi hizo zililenga mikoa 14 yenye maambukizi makubwa ya malaria Tanzania Bara na mikoa yote mitano ya Zanzibar, ikiwa ni asilimia 57 ya watu wote wa Tanzania.

Mshauri wa Mpango wa PMI nchini Tanzania, Naomi Serbantez amesema kwa kukuza utaalamu wa ndani na kutumia maarifa yanayotokana na takwimu, mradi huo umeweka msingi wa maendeleo endelevu katika kutokomeza malaria kote Tanzania Bara na Zanzibar.

Mafanikio muhimu yalijumuisha kuimarisha uwezo wa mashirika ya usambazaji wa vifaa vya matibabu ya Tanzania kusimamia usambazaji wa vyandarua kwa uhuru, kuboresha vifaa vya usafirishaji kupitia zana za kisasa na mifumo ya kufuatilia kwa wakati halisi na kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu wa juhudi za kuzuia malaria.