Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vitambulisho Nida kuanza kutolewa mwezi huu

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) zili-zopo Kawe jijini, kwa ajili ya kujiandikisha ili wapate vitambulisho vya Taifa.

Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Januari hii ndiyo mwisho wa tatizo la uhaba wa vitambulisho vya Taifa (Nida), litakapopatiwa ufumbuzi na kuanza kutolewa kwa wingi.

Kiongozi huyo amesema kilichochelewesha kufikia hatua hiyo mapema ni mchakato wa manunuzi ndani ya Serikali ambao ulikuwa na vipengele vingi.

Alisema mashine hiyo hainunuliwi ikiwa imefungwa pamoja, bali kila sehemu ya utendaji kazi ndani yake inakuwa na mkataba wake na itafungwa kati ya Januari 20 hadi 25, 2021.

Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo jana alipoulizwa na Mwananchi kuhusu lini tatizo la uhaba wa vitambulisho litakwisha na nini chanzo chake.

Msingi wa swali hilo ulitokana na ukweli watu waliojiandikisha wamekuwa hawapati vitambulisho kwa muda badala yake wanapewa tu namba, huku maeneo mengine hata namba zenyewe hawajazipata.

Simbachawene alikiri kuwepo kwa tatizo hilo akisema hata yeye linamkwaza kuona Watanzania wanakosa vitambulisho ambavyo ni muhimu, lakini akataja changamoto ambazo zimekwamisha.

“Mashine tuliyo nayo inafanya kazi kizamani sana, kumbuka tunazalisha vitambulisho 2000 kwa siku kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na idadi ya Watanzania waliotambuliwa, lazima tubadilike,” alisema Simbachawene.

Waziri alisema idadi ya Watanzania waliokuwa wametambuliwa hadi mwishoni mwa mwaka 2020 walikuwa 18.5 milioni, lakini waliopewa vitambulisho walikuwa 6.3 milioni tu na kwamba watu 12.2 milioni walikuwa hawajavipata.

Suluhu ya tatizo hilo alisema ni mashine mpya itakayofungwa ambayo itakuwa na uwezo wa kuzalisha vitambulisho vingi kwa wakati mmoja.

Alisema mkataba walioingia wakati wa kununua mashine mpya, ulionyesha ingezalisha vitambulisho 50 kwa dakika, lakini matokeo katika majaribio iliweza kuzalisha vitambulisho 45 kwa dakika, hivyo ilibidi kurudi upya katika mkataba jambo lililochukua muda.

Kutokana na malengo hayo mashine hiyo itazalisha vitambulisho 43,200 kwa siku, ikiwa ainaafanya kazi kwa saa 16 kila siku. .

Na ikiwa watafunga mashine yenye uwezo wa kuzalisha vitambulisho 45 kwa dakika na ikafanya kazi saa 16 yaani nane mchana na nane usiku kama alivyoeleza, itachukua siku 283 ambayo ni sawa na miezi 10 kumaliza vitambulisho kwa Watanzania waliosalia.

Hata hivyo, ikiachwa mashine ya zamani kuendelea na uzalishaji wa vitambulisho 2,000 kwa siku, itachukua siku 6,250 ambazo ni sawa na miaka 17 au miezi 204 ili Watanzania 12.2 milioni waweze kupata vitambulisho vyao.

Waziri alisema licha ya kuwa hawajafunga mashine mpya, uzalishaji wa vitambulisho haujawahi kusimama na hivi karibuni wametoka kupeleka vitambulisho 20,000 katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na maeneo mengine wanaendelea kupeleka kadri wanavyochapisha.

Akijibu kuhusu malalamiko yanayotolewa ikiwemo taarifa kwenye mitandao kuhusu wananchi wa Karagwe kupata shida ya kupewa namba, alisema taarifa hizo anazo na kwamba anafuatilia kwa wahusika ili aweze kulifanyia kazi.

Mapema mwaka jana akiwa na siku chache tangu alipoteuliwa kwa wadhifa huo, Simbachawene alitangaza kuwaondoa baadhi ya watumishi katika mamlaka ya vitambulisho aliosema hawaendani na kasi inayotakiwa na mara kadhaa walitajwa kuwa na lugha chafu.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Simbachawene alisema jumla ya Watanzania 21,823,026 walikuwa wamejitokeza na kujisajili hadi Machi 27, 2020 kati ya watu 27,796,983 waliotarajia kusajiliwa.