Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unywaji maziwa bado unasuasua Tanzania

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imesema, usindikaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita milioni 75.9 mwaka 2021 hadi Lita Milioni 77.6 kwa mwaka 2022.

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema, usindikaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita milioni 75.9 mwaka 2021 hadi Lita Milioni 77.6 kwa mwaka 2022.

Hatahivyo, Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya kutoka bodi ya Maziwa, Profesa Zacharia Masanyiwa alisema bado kiwango cha unywaji maziwa kilichopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Chakula Duniani (FAO) hakiridhishi.

Profesa Masanyiwa alisema kwa wastani mtu mmoja anakunywa lita 62 za maziwa kwa mwaka wakati kiwango kinachoshauriwa na wataalam hao ni lita 200 kwa mwaka.

Hayo yalijili jana Alhamis Septemba 28, 2022 wakati akizungumza kwenye siku ya maadhimisho ya unywaji maziwa shuleni ambayo huadhimishwa kila Jumatano ya mwisho ya mwezi Septemba.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alisema ongezeko hilo la usindikaji limechangiwa na kasi ya uanzishwaji wa vituo 238 vya ukusanyaji wa maziwa kwenye maeneo yenye mfumo wa masoko unaounganisha viwanda vya usindikaji wa maziwa.

“Nitoe rai kwa wafugaji kuunda ushirika imara ili kupata huduma mbalimbali za mifugo kuongeza upatikanaji wa masoko na usindikaji wa maziwa,” alisema.

Serikali imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kuwataka kunywa maziwa yaliyosindikwa na sio yanayouzwa kwenye chupa za maji barabarani.