Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulaji mayai wapungua nchini

Ulaji mayai wapungua nchini

Muktasari:

  • Kiwango cha ulaji wa mayai nchini kwa mtu mmoja kwa mwaka kimeshuka kutoka mayai 300 hadi mayai 106.

Moshi. Kiwango cha ulaji wa mayai nchini kwa mtu mmoja kwa mwaka kimeshuka kutoka mayai 300 hadi mayai 106.

Kauli hiyo imetolewa jana Oktoba 17,2021 na Waziri wa kilimo, Profesa Adolf Mkenda wakati akifunga maadhimisho ya kilele cha siku ya chakula duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro

"Ulaji wa mayai nchini kwa mtu kwa mwaka ni mayai 106 ,kiwango hiki ni cha chini ukilinganisha na kiasi kinachopendekezwa ambacho ni mayai 300 kwa mtu kwa mwaka," amesema Profesa Mkenda.

Profesa Mkenda amesema walaji wa mayai ni wale wenye kipato cha juu na cha kati ambapo wengi wao ni waliopo maeneo ya mijini na vyuoni.

Amesema pamoja na kiwango ulaji wa mayai kuwa chini, uzalishaji wake umeongezeka kutoka bilioni 3.58 kwa mwaka 2019/20 hadi 4.5 kwa mwaka 2020/21 sawa na ongezeko la asilimia 26.

Profesa Mkenda amesema ongezeko hilo la uzalishaji linatokana na kuongezeka kwa vituo vya kutotoleshea vifaranga vya kuku kutoka vituo 26 kwa mwaka 2019/20 hadi vituo 28 kwa mwaka 2020/21 na wananchi wamehamasika katika kufuga kuku.

"Nawasihi wafugaji na wakulima muendelee kujifunza teknolojia mbalimbali ambazo zinaweza kuongeza uzalishaji wa mayai hapa nchni,"amesema Profesa Mkenda