Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uislam na huduma kwa wenye mahitaji maalumu

Muktasari:

  • Mtume Muhammad (Rehema na amani ziwe juu yake) alikataza kabisa kuwadhalilisha au kuwadharau watu wenye ulemavu.

Dar es Salaam. Uislamu umetambua haki kamili na ya kina ya watu wenye mahitaji maalum, na ukaweka nafasi yao juu katika jamii ya Kiislamu.

Aidha, Uislamu umehimiza kuwaheshimu wale walio na vipaji, maarifa, kazi za manufaa au waliopitia uzoefu wa mafanikio.

Mtume Muhammad (Rehema na amani ziwe juu yake) alikataza kabisa kuwadhalilisha au kuwadharau watu wenye ulemavu.

 Hii ni kwa sababu mtu aliyepatwa na mtihani huo anaweza kuwa na daraja kubwa zaidi mbele ya Allah Mtukufu, au kuwa na fadhila, elimu, juhudi katika jihadi, uchamungu, heshima, na maadili bora kuliko wengine.

Jamii ya Mtume wa Allah ilikuwa inashirikiana na kushikamana katika kuwafariji na kuwaheshimu watu wenye mahitaji maalum, kwa kufuata mfano bora wa Mtume katika kuwahudumia na kuwapa heshima inayostahili.

Uislamu umeamrisha kutembelea wagonjwa kwa ujumla, na hasa wale wenye ulemavu, kwa lengo la kuwafariji na kupunguza mateso yao. Hii ni kwa sababu mtu mwenye ulemavu huwa katika hatari ya kujitenga, kukata tamaa, na kuangalia maisha kwa mtazamo wa huzuni.

Uislamu umwewapa haki za kipekee

Uislamu haukukomea tu kwenye kuhakikisha haki kamili kwa watu wenye mahitaji maalum, bali pia umeipa fursa hii kipaumbele.

 Mahitaji yao yanapewa nafasi ya kwanza kuliko ya watu wasio na ulemavu. Huduma kwao inatangulizwa kuliko huduma kwa watu wa kawaida. Kisa cha Abdallah bin Umm Maktum (Allah Amridhie) ni ushahidi wa wazi. Alimjia Mtume wa Allah akiuliza kuhusu jambo la dini, wakati Mtume alikuwa ameketi na baadhi ya wakubwa wa  kabila la Kuraish, akiwalingania Uislamu huku akitaraji kusilimu kwao kutarahisisha wafuasi wao kusilimu kwa wingi.

Ingawa Abdallah hakuona wala kugundua kuwa Mtume  wa Allah hakumjali kwa muda, lakini Allah Mtukufu aliteremsha aya zenye maonyo makali dhidi ya Mtume wake akilaumu kitendo hicho, Allah Mtukufu anasema: "Alikunjia uso  (mtume wa Allah) na kugeuka .Kwa sababu alimjia kipofu (Abdallah) . Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?  Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? " (80: 1–4).

Baada ya tukio hilo, Mtume  wa Allah alikuwa akimkaribisha Abdallah kwa bashasha, akimfariji na kumwambia: "Karibu ewe mtu ambaye kwa ajili yako Mola wangu alinilaumu."

Kisa hiki kinadhihirisha kuwa kumtanguliza mwenye ulemavu katika kumtimizia haja yake ni jambo lenye uzito wa kisharia, na linapaswa kupewa kipaumbele mbele ya mahitaji ya watu wengine.

Mtume  wa Allah aliwapa heshima, faraja na matumaini wale waliopatwa na ulemavu au maradhi. Aisha (Allah Amridhie) alisema: “Nilisikia Mtume wa Allah akisema:

 ‘Hakika Allah– Azza wa Jalla – alinifunulia (aliniteremshia wahyi) kuwa yeyote anayefuata njia ya kutafuta elimu, humrahisishia njia ya kwenda peponi. Na yule anayepokonywa macho yake mawili (yaani kipofu), nitamlipa Pepo kwa ajili ya (macho) hayo.’”

Amru bin Al-Jamuh (Allah Amridhie) alikuwa mlemavu wa mguu siku moja Mtume alimwambia: "Nakuona kana kwamba unatembea kwa mguu huu ukiwa mzima kabisa huko Peponi " Ibn Umm Maktum alipewa nyadhifa na Mtume Ingawa ni kipofu Mtume alimfanya kaimu wake mjini Madina mara mbili, ili aongoze watu kwenye swala kahalika alikuwa mwadhini wa Mtume wa Allah.

Uislamu umehimiza kuwatembelea wagonjwa kwa ujumla, na hasa wenye ulemavu, ili kupunguza mateso yao ya kimwili na kisaikolojia.

Hili linatokana na ukweli kuwa mtu mwenye ulemavu huwa karibu zaidi na hali ya kujitenga, huzuni, na msongo wa mawazo kuliko mtu mwenye afya njema. Ni kosa kuwaacha au kuwasahau watu hawa katika hafla za kijamii kama ndoa au mikutano. Mtume alikuwa akiwatembelea wagonjwa, kuwaombea dua, kuwatia moyo, kuwapa matumaini, na kueneza furaha katika nyoyo zao. Alifika hadi pembezoni mwa mji kumtembelea mtu mmoja ili tu kumtosheleza haja ndogo au kuswali nyumbani kwake.

 Kwa mfano, Itbaan bin Malik  (Allah Amridhie) aliyekuwa kipofu, alimwambia Mtume: “Laiti ungenijia ukaswali nyumbani kwangu ili sehemu hii niifanye ya kuswalia.” Mtume alimwahidi kwa kusema kwa unyenyekevu: “Nitafanya hivyo In Shaa Allah.”

Katika huruma yake, Mtume aliwafanyia dua watu wenye mahitaji maalum, kuwapa msukumo wa kusubiri majaribu yao kwa subira na azma. Mwanamke mmoja aliyekuwa akipatwa na kifafa alimuuliza Mtume: “Napatwa na kifafa na hujitokeza mwilini mwangu, basi niombee.” Mtume akamwambia: “Ukipenda, subiri na utapata Pepo; na ukipenda, nikuombee upone.” Akasema: “Nitasubiri, lakini niombee nisifunuke (nguo zangu za mwilini).” Mtume akamuombea.

Hivyo ndivyo jamii ya Kiislamu inavyopaswa kuwahurumia wenye ulemavu, kwa kufuata mfano wa Mtume wa rehema.

Mtume alionya kwa ukali sana dhidi ya kumdhulumu au kumdhalilisha mtu kipofu kwa kumtendea kwa dharau au kejeli.

 Amesema: “Amelaaniwa anayempoteza kipofu njia yake.” Hili ni onyo kali kwa yeyote anayewabeza watu wenye ulemavu kwa mzaha, dhihaka au kuwanyanyapaa.

Watu hawa ni ndugu zetu waliojaribiwa na Allah, na si vema kuwafanya kuwa kichekesho, bali tuwaone kama fundisho la uwezo wa Allah.