TRA yaanzisha vituo maalum Kariakoo

Baadhi ya wateja wakiwa katika kituo cha TRA kilichopo mtaa wa Aggrey/Likoma wakipatiwa huduma.
Muktasari:
- Mamlaka ya Mapato mkoa wa kikodi Kariakoo umesama vituo vitatu vilivyoanzishwa vinalenga kuwasogezea wateja wao huduma na kupunguza msongamano katika kipindi hiki cha kuelekea kufunga Mwaka wapili wa mlipakodi.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato, (TRA) mkoa wa kikodi Kariakoo imesema vituo vitatu vilivyoanzishwa vinalenga kuendelea kuboresha huduma kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
Vituo hivyo vitatu vimefunguliwa havitakuwa vya kudumu kwani vitafanyakazi kwa siku kumi na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kulipa kodi katika kipindi wanachoelekea kufunga Mwaka wapili wa Kodi utakao malizika Juni 30 Mwaka huu.
Meneja msaidizi wa TRA mkoani hapo,Tilson Kabuje, amesema vituo hivyo vitasaidia kupungumza msongamano wa watu katika Ofisi za makao makuu ya mkoa huo huku akieleza utaratibu huo wamekuwa wakifanya kila Mwaka.
"Vituo hivi vinalenga kuendelea kuboresha huduma kwa kuwasogezea karibu wateja wetu kwa kutoa elimu na kuwakumbusha wajibu wa kulipa kodi na vilevile tunaepusha msongamano katika Ofisi Kuu kwakuwa kipindi cha kufunga Mwaka kikodi Kuna kuwa msongamano wa watu," amesema Kabuje.
Kwa upande wake, mmoja wa mtoa huduma katika vituo hivyo, Amos Kalongola amesema wengi wanaotembelea katika vituo hivyo ni vijana.
"Na wengi wanahitaji zaidi Tin namba lakini changamoto iliyopo wanaohitaji unakuta hawana namba za kitambulisho cha Taifa, cha mpiga kura na barua ya utambulisho kutoka serikali za mtaa, " amesema.