Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simbachawene ataka vijana wafundishwe kujitegemea

Waziri wa Nchi, Ofidi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amekitaka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kuwa kielelezo kwa kuzalisha wahitimu bora.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema msingi mzuri wa elimu unahitaji kumjenga muhitimu kuwa na uwezo wa kuchanganua na kukabiliana na changamoto katika jamii.

Katika kauli yake hiyo, Simbachawene alikitaja Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kuwa kielelezo sahihi cha kuzalisha wahitimu wenye uhalisia huo.

Simbachawene ameyasema hayo leo Septemba 22, 2023 alipofungua kikao cha wahitimu wa OUT katika hafla ya mikutano wa pili wa Jumuiya ya Wahitimu wa chuo hicho.

Ameeleza utaratibu wa mafunzo katika chuo hicho ni kujitegemea kwani mwanafunzi hujitafutia mahitaji ya kujisomea, mazingira ambayo yanafanana na atakayokutana nayo kazini.

“OUT mwanafunzi anafundishwa kujitegemea kwa kutafuta mahitaji yote yampasayo kusoma, mazingira hayo ndio anayokutana nayo kazini," amesema.

Hata hivyo, amesema kulingana na utaratibu wa chuo hicho, hata wafanyakazi ni rahisi kujiendeleza bila kuathiri shughuli zao.

"Kwa watu waliokosa fursa ya kupata elimu ya juu kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwemo kubanwa na majukumu ya kazi OUT ni fursa kwao. Mimi nilikuwa nafanya shughuli zangu huku najiendeleza kielimu kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na nikahitimu vizuri," amesema.

Rais wa Jumuiya ya Wahitimu wa chuo hicho, Mussa Sima amesema utaratibu uliopo unamwezesha mfanyakazi kusoma huku akiendelea na majukumu yake, badala ya kusitisha kazi kwa ajili ya masomo.

“Imetusaidia sana. Mtumishi aliyepo kazini badala ya kuacha kazi na kwenda kusoma, sasa ana nafasi ya kupata elimu ya chuo kikuu na bado anaendelea na majukumu ya kazi yake. Hii inamsaidia kuongeza ujuzi na kukua katika ajira kiutumishi,” alisema Simba ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini.

Makamu Mkuu kuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda amesema mkutano huo ni mwanzo wa ushirikiano kati ya chuo na jumuiya ya wahitimu.

“Tunawahitaji wahitimu wafanye kazi ya kutangaza huduma zetu kwa jamii, tunawahitaji kwa kupata taarifa za maendeleo ya elimu yao baada ya kuhitimu ili tuimarishe mitaala yetu,” amesema.