Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kumwaga ambulance 258 nchi nzima

RAIS SAMIA AKIZINDUA MFUMO WA USAFIRISHAJI WA DHARURA WA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA (M-MAMA)

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amesema magari ya wagonjwa 233 ya kawaida yanatarajiwa kumwagwa Tanzania nzima, huku mengine 25 zenye hadhi ya rufaa pia yakitarajiwa kuwasili.


Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema magari ya wagonjwa 233 ya kawaida yanatarajiwa kumwagwa Tanzania nzima, huku mengine 25 zenye hadhi ya rufaa pia yakitarajiwa kuwasili.

Rais Samia ameyasema hayo leo Aprili 6, 2022 katika uzinduzi wa mfumo wa usafirishaji wa dharula kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Vodacom.

Rais Samia amesema pamoja na jitihada zote zinazofanywa na Serikali lakini pia imejithidi kuhakikisha kuwa walau kila kata inakuwa na gari moja la wagonjwa.

“Tumeagiza ambulance 233 za kawaida ambazo zitamwagwa Tanzania nzima lakini pia tumeagiza ambulance 25 kama ngazi ya rufaa ile ya kawaida ikiwa haitoshi haina vifaa basi hizo ni zitatumika maana zinafanana na kituo cha afya ngazi ya kata,” amesema Samia.

Amesema pia wameagiza magari 242 za uratibu huku akieleza kuwa ni matumaini yake kuwa zitakwenda kuongeza nguvu katika mpango wa M-mama ili kuwawahisha watoto na kinamama hospitalini.

Amesema kukamilika kwa anuani za makazi pia kutasaidia kuweka urahisi wa uchukuaji wa wagonjwa kwenye maeneo yao kwenda hospitalini kutokana na urahisi katika kuelekeza.