Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ongezeko la wanafunzi shule la binafsi


Muktasari:

  • Takwimu za mwaka 2024 zinaonyesha kuwa wanafunzi waliojinga kidato cha kwanza kwenye shule za Serikali walikuwa 981,013 na mwaka uliofuata 2025 walipungua hadi 889,315; wakati wale wa shule za sekondari za binafsi waliongezeka kutoka 75,776 mwaka 2024 hadi 83,188 sawa na ongezeko la asilimia 9.8.



Dar es Salaam. Mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia, ufaulu na elimu inayotolewa vimetajwa kuwa sababu ya idadi ya wanafunzi katika shule za binafsi kuongezeka wakati wanafunzi wa shule za Serikali wakipunguza.

Hiyo ni baada ya taarifa kuonyesha kupungua kwa wanafunzi wanaoandikishwa katika shule za aerikali waliodahiliwa kwa darasa la awali na kidato cha kwanza kati ya mwaka 2024 na 2025.

Taarifa hiyo inaonyesha mwaka 2025, wanafunzi 1,656,726 waliandikishwa katika elimu ya awali ambapo 1,523,955 walikuwa wa shule za sSerikali ikilinganishwa na wanafunzi 1,558,549 walioandikishwa mwaka 2024, sawa na upungufu wa asilimia 2.2.

Aidha, wanafunzi walioandikishwa katika shule zisizo za Serikali walikuwa 132,771 mwaka 2025 ikilinganishwa na wanafunzi 118,010 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 12.5.

Takwimu hizo zilizobainishwa na ripoti ya Hali ya Uchumi 2025, zinatajawa kuchangiwa na kuongezeka ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa elimu kufuatia maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 iliyoboreshwa mwaka 2023.

Katika upande wa kidato cha kwanza mwaka 2024 wanafunzi wa shule za Serikali walikuwa 981,013 ambao walipungua hadi 889,315 mwaka 2025, sawa na asilimia 9.3.

Katika kipindi hicho, wanafunzi wa shule za sekondari za binafsi waliongezeka kutoka 75,776 mwaka 2024 hadi 83,188 sawa na ongezeko la asilimia 9.8.

Akichamabua takwimu hizo, Mwalimu Richald Mabala amesema udahili katika shule za awali unaweza kuchangiwa na ongezeko la vituo vya kufundishia watoto vinavyofunguliwa katika maeneo tofauti huku vikitumia lugha ya Kiingereza.

Suala hilo limewavuta wazazi wengi na kuwafanya wapeleke watoto wao hata kama Kiingereza kinachotumika si kizuri, kwani wengi wanaamini lugha hiyo itawafanya watoto wafanikiwe.

Hata hivyo, amesema wazazi wameendelea kuchagua kupeleka watoto wao katika shule za binafasi kwa sababu kuna vitabu na vitu vingi vya kuchezea, kuliko shule nyingi za Serikali.

“Pia miundombinu ni mizuri zaidi na matokeo ya kidato cha nne ukiacha shule zile za vipaji za serikali matokeo ya shule binafsi ni mazuri zaidi,” amesema.

Kwa upande wa madarasa, amesema yale ya shule binafsi yana wanafunzi wachache, walimu wa kutosha, wastani wa wanafunzi kwa darasa uko sawa, hivyo wazazi wanakuwa na matumaini kuwa wakiwapeleka watoto wake kwenda shule binafsi atapewa uangalizi wa karibu zaidi ikilinganishwa na shule za Serikali.

Jambo hili linafanya wazazi wengi sasa kunaangalia uwezo wa mtoto kupata elimu inavyotakiwa si suala la wao kuwa na uwezo wa kifedha tena, kama ambavyo imekuwa ikionekana,” amesema.

Amesema jambo hili linapaswa kubadilishwa kwani kwa nchi ambazo zimefanikiwa ziliamua kuwekeza sana katika elimu.

“Tunaweza kuondokana na hili kwa kuwekeza katika maandalizi ya walimu, mfano Rwanda baadhi ya shule binafsi zinafungwa kwa sababu wazazi hawaoni haja ya kupeleka watoto huko kwani shule za Serikali zinatoa elimu nzuri,” amesema.

Hoja za Mabala zinaungwa mkono na Samira Masanja, mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam ambaye alichagua kumpeleka mtoto wake shule ya binafsi kwa kuzingatia ubora wa elimu na usalama wa mtoto anapokuwa shuleni.

Amesema kutokana na kubanwa na majukumu ya kazi alilazimika kuchagua shule ambayo mtoto wake anasoma ili awe na uhakika wa kwenda shule na kurudi chini ya usimamizi mzuri, kwani anachukuliwa nyumbani na kurudishwa nyumbani.

“Pia ubora wa elimu inayotolewa, hata kama shule ya Serikali ingekuwa karibu na makazi yangu bado ningechagua shule binafsi kwa ajili ya elimu nzuri atakayopata mtoto wangu,” amesema.

Mtafiti wa elimu, Dk Muhanyi Nkoronko amesema watu wengi wameanza kuhamia shule binafsi kwa sababu wanaona elimu inayotolewa ni bora zaidi kuliko shule za Serikali, ikichangiwa na uwekezaji uliofanywa na wawekezaji hao.

Amesema baadhi ya shule zimekuwa na mazingira bora ya ufundishaji, vifaa vya kufundishia vinatosha na idadi ya walimu inatosha kuwasimamia wanafunzi.

“Hiyo inafanya mzazi aone kumpeleka mtoto huko atapata elimu bora wkilinganisha na serikalini ambapo kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri ufundishaji wa watoto,” amesema.


Nini kifanyike

Katika mapendekezo ya nini kifanyike, Mabala amesema ni wakati wa kuzifanya shule za Serikali kuwa bora kama zamani ambapo watoto waliochaguliwa huko waliona fahari kutokana na ubora uliokuwapo.

“Kuwekeza zaidi katika shule za Serikali, tuangalie bajeti ya elimu ikoje kama inaongezeka, walimu wako mitaani na upungufu wa walimu katika shule za Serikali bado upo mkubwa, tuangalie vipaumbele vyetu kuhakikisha elimu yetu inakuwa sawa,” amesema Mabala.

Ili kufanikisha hayo, Mabala amesema: “Tupenge upya bajeti ili kuhakikisha kipaumbele kikubwa kinaenda kwenye elimu sambamba na kuwa mitalaa inayolenga kesho siyo leo, kwani watoto wa kidato cha kwanza hadi wanamaliza kazi nyingi zitakuwa zimeondolewa na teknolojia,” amesema.


Serikali inafanya nini

Ili kupunguza baadhi ya changamoto kwenye shule zake, Bajeti ya Elimu iliyowasilishwa na Waziri wake Profesa Adolf Mkenda imebainisha itaendelea kuongeza miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi na sekondari.

“Hili litafanyika kwa kuwezesha ujenzi wa madarasa 1,360 kwa ajili ya utekelezaji wa elimu ya miaka 10 ya lazima, mabweni 17 kwa shule za sekondari 17, nyumba 33 za walimu na  itawezesha ujenzi wa vituo 50 vya walimu katika halmashauri za wilaya.