Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruto: Mambo ya kesho mahakamani tumemuachia Mungu

Muktasari:

  • Ikiwa imebaki saa chache kufikia siku ya hahukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya urais wa Kenya, Rais mteule William Ruto amesema mambo ya kesho mahakamani wamemuachia Mungu na viongozi wa mahakama.

Nairobi. Ikiwa imebaki saa chache kufikia siku ya hahukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya urais wa Kenya, Rais mteule William Ruto amesema mambo ya kesho mahakamani wamemuachia Mungu na viongozi wa mahakama.

Pia, Ruto amewataka Wakenya kumuombea Rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta kusimamia kwa busara kipindi hicho cha mpito katika Taifa hilo.

Ruto ambaye ni Naibu Rais wa Kenya amesema hayo leo Jumapili Septemba 4, 2022 ikiwa ni siku moja kabla ya Mahakama ya Juu ya Milimani nchini Kenya kutatoa uamuzi wa kesi hiyo, akisema kuwa wamemuachia Mungu na viongozi wa mahakama waamue ili Kenya iweze kwenda mbele.

“Sisi ni watu ambao tunamtambua Mungu na hata maneno ya kesho mahakamani tumemuachia Mungu na tumewaachia viongozi wetu wa mahakamani waamue ili Kenya iweze kwenda Mbele” amesema Ruto

Amesema kuwa Wakenya wanatarajia kuwa na kipindi cha mpito chenye amani ili Taifa hilo liweze kusonga mbele.

 “Mimi ninachowaomba kwa heshima kubwa tumuombee Rais wetu Uhuru Kenyetta katika wakati huu wa ‘transition’, Mungu ampatie hekima ili tuweze na transition ya amani”

Kesho Jumatatu, Jaji Mkuu Martha Koome na majaji Philomena Mbete Mwilu, Mohamed Ibrahim, Dk Smokin Wanjala, Njoki Susanna Ndung’u, Isaac Lenaola na William Ouko wanatarajiwa kutoa uamuzi wao kuhusu kesi ya kupinga ushindi wa rais mteule Ruto iliyofunguliwa na Raila Odinga na baadhi ya watu wakipinga matokeo ya urais yaliyotangazwa na IEBC

Uamuzi wa kesi hiyo utatoa uelekeo kama kama Ruto ataapishwa Septemba 13, 2022 kuwa Rais wa Kenya au kinara wa Azimio la Umoja, Raila Odinga atapata fursa nyingine ya kuwania urais kama matokeo yatabatilishwa au atakwenda kustaafu siasa.

Majaji hao wamejifungia kuandaa hukumu ya kesi hiyo tangu Ijumaa baada ya mawakili wa pande zote kuhitimisha uwasilishaji wa ripoti zao za mwisho katika jitihada za kushawishi majaji hao saba kukubaliana na misimamo yao katika kesi hiyo.

Katika matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Agosti 15 mwaka huu, Ruto alishinda kwa kuzoa kura 7, 176, 142 (asilimia 50.49 ya kura) huko Odinga alipata kura 6, 942, 930 (asilimia 48.85).