Rose Manfere ndiye Miss Tanzania 2020

Rose Manfere ndiye Miss Tanzania 2020

Muktasari:

Mshiriki aliyekuwa akiwakilisha  Kanda ya Dar es Salaam, Wilaya ya Kindoni Rose Manfere ndiye Miss Tanzania.

Dar es Salaam. Rose Manfere mwenye miaka 21 ametangazwa kutwaa taji la Miss Tanzania usiku wa kuamkia leo Jumapili Desemba 06, 2020.


Rose Manfere ndiye Miss Tanzania 2020


Nafasi ya pili imenyakuliwa na mrembo Juliana Rwehimiza na nafasi ya tatu akiibeba  Prisca lyimo.

Kutokana na ushindi huo, Rose amezawadiwa gari aina ya Toyota Subaru Impreza toleo la Mwaka 2011 lenye thamani ya Sh13 milioni.

Wakati mshindi wa pili Juliana ataondoka na seti ya sofa na meza ndogo ya sebuleni.

Mashindano hayo yaliyoanza Saa 4:00 usiku, yalihitimishwa Saa 8 usiku na mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.