Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Moro awapa mbinu wakurugenzi kuvutia wawekezaji

Wadau wa uwekezaji mkoani Morogoro wakiwa kwenye mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji katika mkoa huo na kuangalia namna ya kumaliza changamoto zinazokwamisha uwekezaji. Picha Hamida Shariff, Mwananchi

Muktasari:

  • Asema vitu vinavyoweza kuvutia watalii ni pamoja na hoteli ambazo amesema zikiwepo kwenye maeneo hayo zitatoa fursa kwa watalii kupenda kwenda kwenye vivutio vilivyopo kwa kuwa wataweza kupata malazi yaliyo bora.

Morogoro. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (RC), Adam Malima amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri kwenye maeneo yanayopakana na vivutio vya utalii kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji ili kuvutia watalii.

Malima ametoa agizo hilo leo Februari 20, 2025 kwenye kikao kilichowakutanisha wawekezaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kinachoelezea fursa za uwekezaji zilizopo mkoani humo na changamoto zilizopo.

Malima amesema vitu vinavyoweza kuvutia watalii ni pamoja na hoteli ambazo amesema zikiwepo kwenye maeneo hayo zitatoa fursa kwa watalii kupenda kwenda kwenye vivutio vilivyopo kwa kuwa wataweza kupata malazi yaliyo bora.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dk Binilith Mahenge amesema moja ya vivutio vya uwekezaji ni pamoja na kuwepo ardhi iliyopimwa na miundombunu bora ya barabara, maji na umeme.

Hivyo amewataka wakurugenzi wa halmashauri kupima maeneo yote ya kwa ajili ya uwekezaji.

Amebainisha kuwa Mkoa wa Morogoro una ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo kwa sasa upo usafiri wa treni ya SGR utakaoongeza fursa ya uwekezaji.

Naye meneja wa TIC Kanda ya Mashariki, Grace Lemunge amesema kituo hicho kwa sasa kimeanzisha dirisha la huduma ya pamoja ambapo wawakilishi wa Taasisi 13 zinazohusika masuala ya uwekezaji wanatoa huduma kupitia dirisha hilo.

"Zamani mwekezaji akija alikuwa analazimika kwenda kwenye taasisi hizo zote kwa ajili ya kukamilisha taratibu ikiwemo, taasisi ya Osha na TBS, hii ilikuwa ni changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakwaza wawekezaji, lakini sasa huduma zote zinapatikana eneo moja," amesema Lemunge.

Katika hatua nyingine, RC Malima amewaonya wawekezaji waliohodhi vitalu vya uchimbaji madini kwa muda mrefu bila kuviendeleza kwamba watu hao watanyang'anywa na kupewa wengine ili kuyaendeleza maeneo hayo.