Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia: Nimeshindwa kufanya PhD

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Alhamishi Januari 27, 2022 anaadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa huku akieleza mambo mbalimbali katika safari yake ya miaka 62.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema alijaribu kufanya Shahada ya Uzamivu lakini kutokana na majukumu mengi ameshindwa huku akisema ataimalizia baadaye.

Mkuu huyo wa nchi amesema hayo leo Alhamishi Januari 27, 2022 wakati wa mahojiano maalumu yaliyorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) yaliyogfanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Rais Samia ambaye leo anaadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, ameeleza mambo mbalimbali tangu alipozaliwa mpaka kuwa Rais huku katika safari yake ya elimu akisema ameishia kwenye shahada ya uzamili (masters) akibainisha kuwa alikuwa na matarajio ya kufanya PhD lakini majukumu yamezidi.

 “Nilijaribu kufanya PhD lakini ukweli ni kwamba pilika ni nyingi nimeshindwa, sijui niseme nimeshindwa au nitaimalizia baadaye, sijui. Labda nitaimalizia baadaye” amesema Rais Samia

Amesema kuwa katika hatua yake ya elimu ya awali mpaka kidato cha nne amesoma shule zisizopungua 10.

“Kuanzia darasa la awali mpaka nimefika kidato cha nne nimesoma shule kama 10 hivi, hiyo ni kwasababu baba yangu alikuwa mwalimu hivyo alikuwa anahamishwa vituo vingi vya kazi, akihamishwa name niko nyuma yake” amesema Rais Samia


Aajiriwa akiwa mtoto

Rais Samia ambaye leo anatimiza miaka 62 amesema kuwa alipata ajira yake ya kwanza lakini kabla ya kuanza kazi alirudishwa nyumbani kwa kuwa bado alikuwa mtoto.

Amesema alipata ajira ya karani masijala mwaka 1977 wakati akiwa na umri wa miaka 17 hivyo ikamlazimu kurudi nyumbani kusubiri kwa muda.

“Niliajiriwa nikiwa mdogo sana mwaka 1977 nikiwa na wa miaka 17 hivi na nakumbuka nilipokwenda kwenye ajira mara ya kwanza wakasema nenda nyumbani, hapa tutafanya child labor kwa hiyo rudi nyumbani, nikarudi nyumbani nikakaa nyumbani miezi sita hivi halafu ndio wakaniita tena”

Amesema kuwa ingawa alipata kazi hiyo lakini aliona kuwa nafasi hiyo hamtoshi hivyo kuamua kwenda kuongeza elimu.

“Niliajiriwa mwaka 1977 nikiwa karani masijala lakini nilikuwa najiona kabisa pale sio mahala pangu, kwa sababu nilikuwa nafanya zaidi kuliko niliowakuta sawasawa na maofisa, na ndicho kilichonifanya niondoke nikaongeze elimu na baada ya kuongeza elimu nikaajiriwa na Shirika la Chakula Duniani, nikafanya kwa miaka tisa” amesema


Jina la Bibi Mchele lampa ushindi ubunge

Akielezea mwanzo wa kuingia kwenye siasa na kilichompo ushindi wa ubunge wa viti maalumu, Rais Samia amesema jina la Bibi Mchele alilopewa wakati akifanya kazi kwenye Shirika la Chakula Duniani (WFP) lilimpa umaarufu kwa wananchi na kumfanya akubalike kwenye ulingo wa siasa.

Amesema kutokana na kufanya kazi kwa ukaribu na wananchi na kuzijua changamoto zinazowakabili alivutiwa kuingia kwenye uwakilishi ili kuwasemea wananchi na kuisimamia Serikali.

“Mwaka 2000 ndio nilipata mawazo ya kuingia kwenye siasa, ukiniuliza kwanini nilikuwa na sababu moja tu, nilikuwa naangalia Baraza la Wawakilishi linavyoendelea, wakati ule upinzania ulikuwa ndio unapamba moto kwa hiyo nikaamua kuingia ili nami niingie kwenye upambanaji” amesema

“Niliamua kuingia niisimamie Serikali na kujibu hoja kwa sababu nilishafanya kazi na wananchi kupitia NGOs kwa hiyo changamoto zote nazijua, sasa unakuta waziri anaulizwa anachojibu ni tofauti na kililichoko kwa wananchi ndio nikaamua niingie kujibu hoja au kupeleka hoja za wananchi”

Amesema kutokana na uhaba uliotokea wakati akifanya kazi Shirika la Chakula Duniani (WFP) alifanya jitihada za kuomba chakula na kupata mchele, samaki na mafuta ya kula ambavyo walivigawa kwa wananchi huku akipewa jina hilo la Bibi Mchele.

 “Nilikuwa sijui mtu anaingiaje, nikauliza nikafahamishwa nikajaribu, nikaenda Kusini ya Unguja nikajitambulisha wengi walikuwa wananijua Bibi Mchele kwa sababu wakati nafanya kazi Shirika la Chakula Duniani (WFP) kulikuwa na tatizo la wadudu kuvamia mazao, kwa hiyo kukawa na uhaba wa chakula lakini kwa sababu niko kule nikafanya jitihada za kuomba chakula kwa ajili ya wananchi”

“Tukapata mchele, samaki na mafuta ya kupikia kwa wingi tukagawa kwa wananchi, kwa hiyo wakanipa jina la bibi mchale, nilipokwenda kujitambulisha wakawa wanasema bibi mchele tunampa, kwa hiyo nikaibuka kuwa mshindi kwenye viti vya wanawake ndio nilipenyea huko” Amebainisha