Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia mgeni rasmi 'Samia Kalamu Awards'

Muktasari:

  • Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinatarajiwa kutolewa April 29, 2025 jijini Dodoma.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ugawaji wa tuzo za wanahabari zinazofahamika kama 'Samia Kalamu Awards'.

Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinatarajiwa kutolewa April 29, 2025 jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 15,2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Dk Rose Reuben amesema wateule takribani 79 wanatarajia kuwania tuzo hizo zenye lengo la kuchochea uandishi wa makala zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi kuhusu maendeleo, uwajibikaji, uzalendo na kujenga chapa na taswira ya nchi ya Tanzania.

Reuben amesema wateule hao walipatikana baada ya kupitiwa na jopo la majaji kwa kazi zilizokusanywa kutoka kwa waandishi wa habari.

"Baada ya kazi hizo kupitiwa na jopo la majaji zilipelekwa kwa wananchi ambao waliwapigia kura na sasa washindi wamepatikana na watakwenda kupatiwa tuzo zao"anasema

Amesema ugawaji wa tuzo hizo umegawanyika katika makundi matatu, kundi la kwanza, linahusisha tuzo maalumu za kitaifa ambazo ni  tuzo ya chombo cha habari mahiri kitaifa, wanahabari wabobevu, Afisa Habari mahiri wa serikali, Mwandishi wa habari mahiri kitaifa, na tuzo ya uandishi wa habari za matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema kundi la pili, linajumuisha Tuzo kwa Vyombo vya Habari ambazo ni Tuzo za Televisheni, Vyombo vya Habari Mtandaoni, Redio ya Kitaifa, Magazeti na Redio za Kijamii.

"Kundi la tatu, ni tuzo za kisekta zitakazotolewa kwa waandishi wa habari waliobobea katika kuandika makala za maendeleo kwenye sekta mbalimbali, "amesema.

Kwa upande Jan Kaaya mhandisi mkuu mwandamizi kitengo cha huduma za utangazaji TCRA amesema washindi watatunukiwa zawadi mbele ya mgeni rasmi kama ishara ya kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika ustawi wa taifa.

"Tamwa na TCRA zinatoa wito kwa waandishi na vyombo vyote vya habari nchini kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha hafla hiyo  ambayo inatoa nafasi kwa wanahabari kutangaza mchango wao kwa jamii na taifa kwa ujumla"anasema