Raia wa Kenya wahukumiwa nchini Tanzania
Muktasari:
- Mahakama ya wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro imewahukumu raia 26 wa Kenya kulipa faini ya Sh500,000 au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kuwakuta na hatia ya kuingia Tanzania bila kuwa na vibali na hati za kusafiria.
Rombo. Mahakama ya wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro imewahukumu raia 26 wa Kenya kulipa faini ya Sh500,000 au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kuwakuta na hatia ya kuingia Tanzania bila kuwa na vibali na hati za kusafiria.
Huku hiyo imetolewa leo Jumatano Machi 10, 2021 na kaimu hakimu mkazi wa Wilaya ya Rombo, Baraka Kibululu.
Awali akiwasomea mashtaka mkaguzi msaidizi wa uhamiaji wilayani humo, Paschal Mayunga amedai Machi 9, 2021 walipata taarifa ya kuonekana kwa watu wasio raia wa Tanzania eneo la Usseri na waliwakamata na kuwafikisha polisi.
Amesema baada ya kufikishwa mahakamani walikiri kutenda kosa hilo, “kwa kuwa washtakiwa wote wamekiri kutenda kosa hilo mahakama inawatia hatiani wote kwa kosa waliloshtakiwa nalo kwa kwenda kinyume na sheria."
"Kwa hiyo kutokana na kutenda kosa hilo mahakama inawahukumu kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh500,000 kila mmoja.”