Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzazi adaiwa kumuua mwanaye kwa kipigo

Muktasari:

Jephta Shome mkazi wa wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, anatuhumiwa kumuua mwanaye Nyanzila Shome (17) kwa madai ya kujihusisha na mapenzi na mtoto wa jirani yao.

Sengerema. Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lusikwi wilayani Sengerema, Nyanzila Shome (17) amefariki dunia akidaiwa kupigwa na mzazi wake Jephta Shome aliyekuwa akimtuhumu kufanya mapenzi wa mtoto wa jirani yake.

Mwanafunzi huyo amekumbwa na mauti hayo siku moja kabla ya kuanza mtihani wa kidato cha pili shuleni hapo.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Maili Makori amesema wanawasaka wazazi wa mtoto huyo waliotoweka mara baada ya mauaji hayo.

Amesema tukio hili lilitokea Oktoba 30 majira ya usiku, ambapo baba wa mtoto (Jephta Shome) anayeelezwa kuwa na tetesi za mwanaye kutembea na mtoto wa jirani yake, alipofika nyumbani alianza kumushambulia mwanafunzi huyo kwa kipigo, hali iliyosababisha kifo cha mtoto huyo.

Makori amewataka watu waache tabia ya kujichukulia sheria mikoni kwa kuwa wanavunja Sheria kwa kusababisha mauwaji yasiyo ya lazima.

"Jeshi la Polisi liko kazini kuwasaka wazazi waike popote walipo na tutawakamata kisha kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” amesema Makori.

Baadhi ya wananchi wilayani Sengerema waliozungumza na Mwananchi, wameeleza kusikitishwa na tukio hilo, huku wakiomba vyombo vya Dola kuchukua hatua kali.

“Tukio hili ni kama miujiza jinsi lilivyotokea, nawaomba wazazi wenzangu kuwa makini pindi tunapotoa adhabu yoyote kwa watoto wao,” amessema Justine John, mkazi wa Kijiji cha Lubanda

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Bunuru Shekidele amesema ndoto za maisha ya mwanafunzi huyo zimeishia ukingoni baada ya kupoteza maisha kwa kupigwa na mzazi wake kitendo ambacho limeleta simanzi kubwa miongoni mwa wananchi.

Shekidele amewataka wazazi kuwa makini wakati wa kuchukuwa maamuzi yoyote wanatakiwa kufanya uchunguzi juu ya tuhuma yoyote inayomuhusu mtu ndipo waweze kuchukuwa hatua.