Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwekezaji aiomba Serikali kubadilisha sharia kuwalinda wazawa

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Dk Ashatu Kijaji akimsikiliza  mtaalamu wa ufundi Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari cha GFA Vehicle Assemblers, Hamadi Ramadhani wakati Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoani Pwani. Picha na Said Khamis

Muktasari:

Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' ameiomba Serikali kurekebisha sheria na kupunguza ushuru ili kuwalinda wawekezaji wazalendo kuweza kushindana na wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi.

Kibaha. Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' ameiomba Serikali kurekebisha sheria na kupunguza ushuru ili kuwalinda wawekezaji wazalendo kuweza kushindana na wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi.

Mereng' ametoa rai hiyo baada ya Kamati ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira ilipofanaya ziara katika kiwanda hicho na kiwanda cha kuzalisha chanjo za mifugo nchini (HESTER Biosciences Africa Ltd).

Pia, ameishauri Serikali kuwaomba waagizaji wa magari (trucks) kuagiza vipuri na kazi ya uunganishwaji ifanyike hapa nichini kuweza kuokoa fedha za kigeni ambazo zingetumika kwa kuagiza magari na badala yake kutanua soko la ajira kwa vujina walioko katika viwanda vya ndani

Kiwand hicho ambacho kipo katika awamu ya pili ya uzalishaji mpaka sasa kimetengeneza magari 420 kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambapo kazi nyingi katika kiwanda hicho hufanywa na watanzania waliopata ujuzi kutoka kwa wataalamu wa kigeni

Kwani kiwanda hicho kina wafanyakazi zaidi ya 100 ambapo kati yao 95 ni Watanzania na 5 ni wageni kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Akijibu baadhi ya hoja zilizotolwea na wawekezaji hao, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Dk Ashatu Kijaji aliwatoa hofu wawekezaji hao akiwahakikishia kuwa Serikali ipo karibu nao na inashughulikia suala la ukatikaji wa umeme ambalo ni miongoni mwa changamoto zilizowasilishwa.

Dk Kijaji amesema Serikali ipo katika hatua za kuongeza vyanzo vya umeme mkubwa ikiwemo mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere ambalo litakuwa mkombozi wa tatizo hilo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Erick Shigongo alisema kamati hiyo italifikisha bungeni suala la kubadilisha sheria kumlinda mwekezaji wa ndani (local content).