Mwalimu mkuu, mtendaji kijiji wakamatwa Tunduru
Muktasari:
Mkuu wa Wilaya yaTunduru, Julius Mtatiro amesema wanawashikilia mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Angalia iliyopo kata ya Mtina wilayani humo na Mtendaji wa Kijiji cha Mtina kwa tuhuma za kupewa fedha ili kuficha taarifa za wanafunzi wawili wa darasa la saba ambao wamepata ujauzito.
Tunduru. Mkuu wa Wilaya yaTunduru, Julius Mtatiro amesema wanawashikilia mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Angalia iliyopo kata ya Mtina wilayani humo na Mtendaji wa Kijiji cha Mtina kwa tuhuma za kupewa fedha ili kuficha taarifa za wanafunzi wawili wa darasa la saba ambao wamepata ujauzito.
Akizungumza na Mwananchi Mtatiro amesema baada ya kubainika wanafunzi hao ni wajawazito mwalimu mkuu akatulizwa na waliowapa mimba na kuwaondoa wanafunzi hao kimya kimya shuleni.
Amesema pia mtendaji wa kijiji naye naye alishiriki kuficha taarifa za wanafunzi haa ambapo hawakuzipeleka kwenye mamlaka yoyote ya ngazi za juu.
Mtatiro amesema kuwa “Baada ya uchunguzi wetu wa kimya kimya tumekamata mtandao wote uliohusika kutengeneza na kuficha njama hizo wakiwemo wazazi, walimu na mtendaji” amebainisha Mtatiro na kuongeza
“Jambo la kusikitisha wazazi, wanaona ni haki yao kupokea mche wa sabuni, sukari pamoja na chumvi kwa gharama ya maisha ya hao mabinti zao na wameeleza kuwa hawaoni shida” amesema
Amesema kuwa baada ya kuzungumza na wanafunzi hao walisema kuwa wanatarajiwa kuolewa na na watu hao walaowapa ujauzito.
”Kama mzazi, kiongozi kunawakati nakutana na mambo ya hovyo lakini na baki kwenye mstari kutokana na miongozo, taratibu za kisheria la sivyo mngesikia DC achapa viboko mabazazi na wabakaji wa watoto,”amesema DC Mtatiro
Kwa upande wake Simon Mhina amempongeza DC Mtatiro kwa kuwa mstari wa mbele kutetea haki za watoto na kuwachukulia hatua wanaoharibu maisha ya watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito.
Mtaalamu wa malezi na makuzi ya mtoto toka Shirika Lisilola Kiserikali (CIC ), Davis Gisuka ameshauri ofisa maendeleo ya jamii waendelee kutoa elimu ili jamii isisababishe madhara ikiwa ni pamoja na kushugulikia kesi hiyo.