Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mti wa ajabu wawa kivutio hifadhi ya Nyerere

Mti wa ajabu wawa kivutio hifadhi ya Nyerere

Muktasari:

  • Mti wa asili uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere umeshindwa kukatika na kubaki katikati ya barabara umekuwa kivutio kwa watalii kwa kutaka kuuona na kuushika kutokana na historia yake kutumiwa kufanya matambiko mbalimbali na jamii.

Morogoro. Mti wa asili uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere umeshindwa kukatika na kubaki katikati ya barabara umekuwa kivutio kwa watalii kwa kutaka kuuona na kuushika kutokana na historia yake kutumiwa kufanya matambiko mbalimbali na jamii.

Mti huo aina ya Marula umekuwa kivutio kwa watu wanaofika kutembelea hifadhi hiyo ambapo mti huo unaelezwa kusaidia mahitaji ya wahusika.

Mti huo umelazimika kuachwa eneo hilo baada ya jitihada za kuukata kushindikana hivyo wajenzi wa barabara waliamua waweke barabara mbili pacha wakati wa upanuzi wa barabara ndani ya hifadhi hiyo ya Nyerere ikitokea Kijiji cha Mloka wilayani Rufiji Mkoani Pwani.

Ofisa Uhifadhi Mwandamizi, Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Seth Mihayo, akizungumzia mti huo alisema umekuwa kivutio kwa sababu wakati wa upanuzi huo wa barabara licha ya kutumia vifaa vya kisasa kama magreda ya kukata miti mikubwa mti huo ulishindikana kukatika na badala yake vifaa hivyo licha ya kuwa vya kisasa lakini viliishia kuharibika na mti kuendelea kubaki.

“Ni kwamba mti huu wakati wa utengenezaji wa barabara walipokuwa wakijaribu kuukata ili kupitisha barabara ilishindikana na kulazimika eneo hili kuwekwa barabara mbili na wenyewe kubaki katikati na sasa umekuwa kivutio kwa watalii wanaofiuka hifadhini,”alisema.

“Baada ya vifaa vyote vilivyotumika kukata mti kuharibika ikiwa pamoja na baadhi ya watu kupotea kimazingira hivyo umepewa jina la mti wa ajabu,”alisema Mihayo.

Ofisa huyo uhifadhi Mwandamizi, amesema walipojaribu kuleta mitambo mingine ya juu zaidi kwa ajili ya kuondoa mti huo pia ilishindikana kuondoa nao ukaishia kuharibika na hivyo kulazimika mtio huo kuachwa katika eneo hilo.

Mihayo amesema baada ya kufanyika kwa utafiti historia inaonyesha kulikuwa na vijiji kipindi cha nyuma ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo kijiji cha Mloka hivyo wazee wa miaka ya nyuma walikuwa wakifanya mambo ya mizimu na matambiko ya kimila na ili kuenzi mila hizo wameamua kuacha mti ili uwe sehemu ya kivutio cha utalii na historia.

“Pamoja na mti huo, hii hifadhi ina kivutio kingine eneo waliokuwa wakiishi mijusi mikubwa katika miaka ya nyuma ambayo kwa sasa mabaki na mifupa yake ilipelekwa Berlin nchini Ujerumani kwaajili ya kuhifadhiwa lakini makazi halisi ya mijusi hiyo katika kipindi cha nyuma ilikuwa ndani ya hifadhi hii ya Nyerere,”amesema.

Mmoja wa Wazee wa eneo hilo kutoka katika Kijiji cha Mloka ambacho kipo jirani na hifadhi hiyo, Mohamed Haule akizungumzia maajabu ya mti huo amesema mti huo wa ajabu umekuwa ukisababisha baadhi ya watu wanaofika katika maeneo hayo kufanya shughuli tofauti na matambiko ikiwemo kuchoma mkaa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

“Katika kipindi cha nyuma yupo mtu mmoja alikwenda katika maeneo ya mti huo kwaajili ya kukata miti na kuchoma mkaa lakini alipotea kwa muda wa siku kadhaa akiwa anazunguka tu maeneo hayo," amesema Haule.

Akizungumzia kuhusu kushindwa kutolewa kwa mti huo wakati wa upanuzi wa barabara, amesema alishuhudia magreda hayo yalivyoshindwa kung’oa mti huo na kuishia kuharibika kimazingara na hivyo kulazimika mti huo kuachwa katikati ya barabara.